Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akisalimia na Miss Tanzania
2011,Salha Israel alieambatana na timu nzima ya Warembo wa Redd's Miss
Tanzania 2012 kwenye ziara ya kutembelea mikoa ya Kanda ya
Kaskazini,wakati waliofika Nyumbani kwa
Waziri Mkuu Mstaafu,Monduli leo kumsalimia na kupata baraka zake kwenye
mashindano hayo.Kuli ni Mkurugenzi wa Rino Agency na Muandaaji wa Miss
Tanzania,Hashim Lundenga na wa pili kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu
Mstaafu,Mama Regina Lowassa.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akisalimia na Msimamizi (Matron) wa warembo wa Redd's Miss Tanzania
2012,Irene Karugaba wakati Warembo hao walipotembelea Nyumbani kwa
Waziri Mkuu Mstaafu,Monduli ili Kupata Baraka zake.Mh. Lowassa
aliwapokea warembo hao kwa furaha na kuzungumza nao machache juu ya
mafanikio ya Mashindano hayo na kuwapa hamasa ya kutokata tamaa hata
mara moja.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akisalimia na Warembo wa Redd's Miss Tanzania
2012 waliofika Nyumbani kwake Monduli leo ili Kupata Baraka zake wakati
wakijiandaa kuelekea kwenye fainali za Shindano hilo zitakazofanyika
Novemba 3,2012 kwenye ukumbi wa Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar es
Salaam.Warembo hao wamekutana na Mh. Lowassa
wakati wakiwa kwenye ziara ya kutembelea Mikao ya Kaskazini na kujifunza
mambo mbali mbali ya Utalii wa ndani.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapa
somo Warembo wa Redd's Miss Tanzania
2012 waliofika Nyumbani kwake Monduli leo.Kushoto ni Mke wake,Mama
Regina Lowassa,Mkurugenzi wa Rino Agency na Muandaaji wa Miss
Tanzania,Hashim Lundenga pamoja na Miss Tanzania wa Sasa,Salha Israel.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiendelea kuzungumza na Warembo hao.
Warembo wakimsikiliza kwa makini Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
Mkurugenzi wa Rino Agency na Muandaaji wa Miss Tanzania,Hashim Lundenga akifafanua jambo kwa Mh. Lowassa na Mama Regina Lowassa.
Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakiwa wamevalia mavazi ya Kimasai.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe
Mama Regina Lowassa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Warembo wanaowania
Taji la Redd's Miss Tanzania 2012 pamoja na Viongozi wa Kamati ya Miss
Tanzania.













No comments:
Post a Comment