Ndugu zangu,
Kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana.
Ona,
moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa
haraka na hata kuteketeza kijiji kizima. Na tangu utotoni
tumetahadharishwa hatari ya kucheza na moto. Naam, binadamu usicheze na
moto, labda iwe kwenye mazingaombwe.
Sisi
sote ni ndugu, na hii ni Nchi Yetu. Hatuna haja ya kubaguana kwa
misingi ya ukabila, dini na rangi. Tuna historia ya kujivunia. Ni
historia yetu wenyewe. Kinyume na baadhi yetu wanavyofikiri au
wanavyotutaka tufikiri, historia yetu haikuanzia enzi za Mwarabu ,
Mjerumani au Mwingereza. Historia yetu haikuanzia enzi za TANU wala Afro
Shiraz.
Na
dini hizi za kimapokeo zinazotufanya sasa tufarakane zimekuja na
kuzikuta dini zetu za asili, na bado tunazo. Na hakika, Afrika
hatugombanii matambiko. Afrika kila ukoo una tambiko lake, hivyo basi,
dini yake. Kamwe hutasikia Waafrika wanagombania matambiko. Hutasikia
Waafrika wakigombana kwa tofauti za matambiko yao.
Na
sisi ni Waafrika. Hii leo mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na
hata kufanikiwa kuwafanya wachinjane ni kwenye kwenye tofauti zao za
imani hizi za kimapokeo; Uislamu na Ukristo.
Naam,
tusifike mahali tukagombana kutokana na tofauti za imani ama dini
ambazo wala si za asili yetu. Imani au dini ambazo, kama ilivyo dini
zetu za asili, nazo zinatutaka wanadamu tuishi kwa amani, upendo na
maelewano.
Na hilo ndilo Neno la leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765, 0754 678 252
http://mjengwablog.com
Thursday, October 25, 2012
Home
Unlabelled
Neno La Leo: Afrika Hatugombanii Matambiko...
Neno La Leo: Afrika Hatugombanii Matambiko...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment