Na Mwandishi Wetu
Bendi ya Mashauzi Classic “Wakali wa Kujiachia” kesho Ijumaa itatambulisha albam yao mpya wakati watakapo tumbuiza katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.
Onyesho hilo limedhaminiwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi.
Mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga amesema kuwa itakuwa ni nafasi pekee kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake kushuhudia utambulisho wa albamu hiyo liitwayo “Viwavijeshi.”
Bendi hiyo inayoongozwa na mwanadada Isha Mashauzipia inatamba na baadhi ya nyimbo kama Si Bure Una Mapungufu, Anayejishuku Hajiamini, Niacheni Nimpende", Mama Nipe Radhi, Nani Kama Mama na Tugawane Ustaraabu .
Mwimbaji nyota wa kundi hicho, Aisha Othman 'Mama Vuvuzela' pia ataimba wimbo wake mpya uitwao, La Mungu Halina Mwamuzi .
No comments:
Post a Comment