HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 25, 2012

katibu wa bakwata mkoa wa Arusha ajeruhiwa kwa bomu


Na Joseph Ngilisho
KATIBU mkuu wa Bakwata mkoani Arusha,Abdulkarim Jonjo (52) mkazi wa Esso jijini Arusha,amenusulika kufa baada ya kujeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospital ya Mkoa Mount Meru baada ya watu wasiojulikana kumlipua kwa bomu la kurushwa kwa mkono akiwa amelala usingizini nyumbani kwake. 

Akiongea kwa taabu katika wodi ya majeruhi hospitalini hapo,Jonjo alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 6.30 usiku akiwa amelala baada ya kuona mwanga wa cheche dirishani kwake na kufuatiwa na kishindo cha mlipuko. 

Alisema kuwa hali hiyo ilimlazimu kuinuka kitandani kuangalia tukio la mwanga huo wa cheche,lakini kabla ya kuufikia alisikia kishindo cha mlipuko mkubwa kilichosababisha kujeruhiwa vibaya baada ya kurushwa umbali ndani ya chumba chake. 

 ‘’unajua jana nilichelewa kulala kutokana na umeme kukatika nilikaa sebuleni hadi saa 5 kasoro dakika 20 nikaenda kulala ,lakini ilipofika majira ya saa 6 kasorobo niliamka kuchaji simu yangu baada ya kuona umeme umerudi na kwenda kulala ,ila ilipofika saa 6.30 ndipo nilisikia cheche dirishani na kufuatiwa na mlipuko’’alisema Jonjo. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus SABAS ameapa kuwasaka waliohusika na tukio hilo linalofananishwa na ugaidi na kuwafikisha mahakamani. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad