WAREMBO 30 wanaowania taji la Redd’s Miss Tanzania 2012 kesho wanatarajiwa kushuka katika ukumbi wa Hoteli ya Giraffe iliyopo Kunduchi, Dar es Salaam kuwania taji la Redds Miss Talent.
Mshindi wa taji hilo atafanikiwa kuingia hatua ya 15 Bora ya Redd’s Miss Tanzania, hivyo kuungana na washiriki wengine wawili ambao wamefanikiwa kukata tiketi hiyo.
Warembo ambao mpaka sasa wamejihakikishia kuingia hatua hiyo ni Lucy Stephano, aliyetwaa taji la Miss Photogenic, Magdalena Roy anayeshikilia lile la Top Model na Mary Chizi aliyetwaa lile la Redd's Miss Tanzania Sports Lady.
Afisa Habari wa Redd’s Miss Tanzania, Haidan Ricco amesema kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni kujua nani ataibuka na ushindi.
“Kutakuwa na burudani kadhaa ambazo zitatolewa na wasanii maarufu hapa nchini, huku washiriki hao wa Redd’s Miss Tanzania nao watatoa burudani za kufa mtu kwa mashabiki.”
Ricco alisema katika shindano hilo linalotarajiwa kuanza saa 2 usiku, huku kiingilio kikiwa ni Sh 15,000 kabla (Steers Mlimani City) na 20,000/- mlangoni.
No comments:
Post a Comment