Mawakili
wa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Abdallah Juma kushoto na Salim Tawfik
wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu nia yao ya kujitoa kwao siku
ya leo katika kesi hiyo kutokana na kile walichoita usumbufu
wanaofanyiwa wateja wao wa kuhangaishwa na kukosa kupelekwa Mahakama ya
Kwerekwe kwa muda muafaka
Kiongozi
wa Jumuiya ya UAMSHO Sheikh Farid Hadi Ahmed kushoto akiwa na wenzake
sita walioletwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga wakiwa hawana ndevu na
kufunguliwa mashtaka manne mapya mahakamani hapo yakiwemo kuharibu mali
za watu zenye thamani ya Shl.Milioni 50 na kufanya vurugu za makusudi
zakuhatarisha amani katika nchi
Baadhi ya Askari wa kutuliza fujo wakiwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga kwa lengo la kulinda usalama na amani Mahakamani hapo
Baadhi
ya Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO wakiwa wanatoka katika Mahakama Kuu ya
Zanzibar Vuga baada ya kufunguliwa mashtaka manne mapya..Picha na
Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Na Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi Zanzibar
VIONGOZI
wanane wa makundi mawili ya Kiislamu Zanzibar wamefikishwa katika
Mahakama Kuu ya Vuga mjini Zanzibar wakituhumiwa na mashitaka manne
yanayohatarisha usalama wa taifa.
Waliofikishwa
katika Mahakama hiyo ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu mjini Zanzibar
Sheikhe Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe,
Mselem Ali Mselem.
Wengine
ni Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis
Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar.
Mbele
ya Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi Mwendesha Mashtaka
wa Serikali, Rayah Mselem alidai katika mahakama hiyo kuwa watuhumiwa
wote kwa pamoja wanatuhumiwa kati ya Oktoba 17 na 18 mwaka huu mchana na
mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, chini ya kifungu namba 16 kifungu
kidogo cha tatu(d) sura ya 47 ya sheria ya Usalama wa Taifa, walitoa
lugha ya uchochezi uliosababisha vurugu, ghasia na kuharibu mali
yakiwemo majengo na barabara.
Mwendesha
mashitaka huyo pia aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa, kati ya Mei
26, na Oktoba 19, mwaka huu, Viongozi hao waliwahamasisha wananchi
mbalimbali wa mji wa zanzibar na viunga vyake kwa maneno ya uchochezi na
kusababisha machafuko yaliyosababisha uhalibifu mkubwa wa mali katika
maeneo mbalimbali ya mji wa zanzibar.
Rayah
ameyataja maeneo ya mji wa Zanzibar yaliyoathiriwa zaidi na machafuko
hayo kuwa ni Lumumba, Msumbiji, Fuoni, Meli Sita na Mbuyuni.
Hata
hivyo watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kutokana na mashitaka
yanayowakabili kuwa ni ya kuhatarisha usalama wa taifa.
Pamoja
na watuhumiwa hao kudai na kuomba dhamana, mahakama hiyo haikuweza
kutoa dhama kutokana na Hati ya iliyowasilishwa mahakamani hapo na
Mkurugrnzi wa mashitaka wa zanzibar ya kuzuia dhamana za watuhumiwa hao
chini ya kifungu namba 19 kifungu kidogo cha (1) na cha pili (2) sura ya
47 ya Sheria ya Usalama wa Taifa iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande hadi Novemba 8, mwaka huu kesi yao itakapokuja tena kwa kutajwa.
Hiyo
ni kesi ya pili kwa watuhumiwa saba na kesi ya kwanza kwa mtuhumiwa hao
isipokuwa kwa mtuhumiwa wa nane Ghalib Ahmed Omari ambaye hiyo ni mara
yake ya kwanza kufikishwa mahakamani.
Mtuhumiwa
Galib ambaye alikuwa akitafutwa na Polisi kwa kuhusika na makosa
yaliyompeleka mahakamani, alikamatwa juzi alipoonekana kwenye maeneo ya
mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe kusikiliza kezi za wenzao.
Mara
walipoondoka katika ukumbi wa Mahakama kuu ya Vuga, washitakiwa wote
saba, walipelekwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe ambako nako
jana pia walipaswa kwenda kusikiliza uwamuzi wa au watapatiwa dhama ama
vinginevyo.
Hata
hivyo mahakama hiyo kesi hiyo imetajwa tu na uwamuzi wa watuhumiwa
kupewa au kutopewa dhama katika kesi hiyo ya kwanza utatolewa Novemba 7,
mwaka huu.
Watuhumiwa hao wamerudishwa rumande katika Gereza la Chuo cha Mafunzo Ziwani.
|
No comments:
Post a Comment