HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 25, 2012

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAZI KWA MAWAZIRI NA MAAFISA WAANDAMIZI WA SERIKALI


Rais Jakaya Mrisho kikwete na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakipitia Waraka wa Utumishi Namba 5 wa mwaka 2009 kuhusu matumizi bora na salama ya vifaa na mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) serikalini wakati wa kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali wanaokutana kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Pamoja naye meza kuu ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali (kulia) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Dk. Jabir Kuwe Bakari, Mtendaji Mkuu, Wakala ya Serikali Mtandao, akitoa mada kuhusu wakala huo kwa wajumbe kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.
Wajumbe wakichangia katika kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali wanaokutana kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yembesi akifafanua juu ya Waraka wa Utumishi Namba 5 wa mwaka 2009 kuhusu matumizi bora na salama ya vifaa na mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) serikalini kwa wajumbe kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad