Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Buttalah akizungumza na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye mkutano wa uzinduzi wa
mashindano ya mbio za mitumbwi ya Balimi ya kanda ya
Ziwa ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza mkoani Kigoma hivi
karibuni.kushoto ni Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager,Edith Bebwa
Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Edith Bebwa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye mkutano wa
uzinduzi wa mashindano ya mbio za mitumbwi ya Balimi ya kanda ya
Ziwa ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza mkoani Kigoma hivi
karibuni.
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo
imezindua rasmi mashindano ya mitumbwi kwa kanda ya ziwa mwaka 2012.
Mashindano
hayo ya kupiga kasia, yanayo dhaminiwa na bia ya “Balimi Extra Lager”
yatashirikisha mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Mara na visiwa vya
Ukerewe.
Mashindano
haya yamekuwa yakijizolea umaarufu katika kanda ya ziwa mwaka hadi
mwaka na yametokea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa na
wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kuongezeka
kila mwaka.
Akiongelea
mashindano ya mwaka huu wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Balimi
Extra Lager Edith Bebwa alisema, Ni zaidi ya miaka saba sasa, bia ya
Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani
Kigoma, kwa kipindi chote hiki Balimi imefanikiwa kuleta changamoto
kubwa katika mchezo wa kupiga makasia, kwa kuwapa fursa wapiga makasia
kutumia mitumbwi yao katika michezo na kujipatia kipato cha ziada
kupitia zawadi nono zinazotolewa lakini pia kuleta burudani kwa wakazi
wanaozunguka ziwa Victoria na lile la Tanganyika.
Kwa
hivi sasa timu zote zimeshaanza maandalizi, tayari kwa mashindano ya
ngazi ya mkoa ambapo kwa mwaka huu yataanzia Kigoma tarehe 20 Octoba,
ikifuatiwa na Kagera tarehe 27 Octoba, Mwanza tarehe 4 Novemba, Kisiwa
cha Ukerewe tarehe 10 Novemba na Mara tarehe 17 Novemba.
Baada
ya fainali hizo za ngazi ya mikoa timu zilizoshinda zitakutana katika
fainali kuu itakayofanyika Jijini Mwanza tarehe 2 Desemba pale Mwaloni
Kirumba.
Akizungumzia timu zitakazofuzu kuingia fainali kuu, Bi Edith alisema;
timu tatu za wanaume na mbili za wanawake zitakazoshika nafasi za juu
zaidi katika ngazi ya mkoa ndizo zitakazoingia katika fainali kuu
itakayofanyika Jijini Mwanza.
Na
timu zilizochukuwa ubingwa mwaka jana upande wa wanaume na wanawake
watapata fursa ya moja kwa moja ya kuingia finali kuu za mwaka huu ili
kutetea ubingwa wao.
Akizitaja zawadi watakazopata washindi katika ngazi za Mkoa na fainali
kuu, Meneja Masoko Bw. Fimbo Butallah alisema;
Kama ilivyo ada, zawadi zimekuwa zikiongezeka kila mwaka, ukiwemo mwaka huu 2012, ambapo zawadi zimepangwa kama ifuatavyo;
Tuna
imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu ya ushindani kwa
washiriki na hivyo kuleta burudani ya aina yake kwa mashabiki.
Tunawaomba wakazi wa kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kujitokeza kwa
wingi kushuhudia mashindano haya yenye mvuto na msisimko wa aina yake.




No comments:
Post a Comment