HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 20, 2012

Mapango ya Amboni Jijini Tanga

Hivi karibuni nilifanya utalii wa ndani katika mapango ya kale ya Amboni huko Jijini Tanga na kufanikiwa kujionea na kujifunza mambo mbali mbali yaliopo ndani ya mapango hayo.kiukweli ndani ya Mapango hayo kuna vivutio ya kila aina na vya kipekee ambavyo ni vya asili ya zama za kale. Miongoni mwa vitu vilivyopo kwenye mapango hayo ni mfano wa sanamu za aina mbalimbali kama za Bikira Maria, Maandiko ya Quran, Daraja, sanamu za jinsia ya kike na kiume, chui, na vitu vingine mbalimbali vya kuvutia.
Katika safari hiyo,sikuwa peke yangu,bali nilikuwa na Marafiki zangu,Erick Othman (shoto) na Mroki Mroki wa Father Kidevu Blog.
Hapa hadithi zikiendelea baada ya kutoka Mapangoni.
Sehemu ya vivutio mbali mbali ndani ya Mapango hayo ya Amboni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad