HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 7, 2012

Kamuzi la Mkali Rick Ross ndani ya Viwanja vya Leaders Club Jijini Dar usiku wa Kuamkia leo

  Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rick Ross akiimba jukwaani  usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye viwanja vya Lidaz Club,wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta likirindima.
 Mkali mwingine wa miduara AT na madansa wake wakilishambulia jukwaa.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,akiimba jukwaani na shabiki wake.
 Mashabiki wakitaka kuangusha uzio uliowekwa kwa ajili ya usalama.
 Baadhi ya Askari wakijaribu kuweka usalama wa kutosha kwa Mwanamuziki Rick Ross mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Lidaz Club,kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
  Mwanamuziki kutoka nchini Marekani,Rick Ross akijisikia furahaa kuwaona Watanzania wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumshuhudia yeye akikamua stejini.
Watu kibao wakiwa ndani ya viwanja vya lidaz club usiku huu.
Msanii wa miondoko ya rusha rohoo a.k.a Miduara,Shilole akijiachia jukwaani vilivyo na madansa wake usiku huu mbele ya umati mkubwa uliofika kwenye viwanja vya Lidaz Club,katika kuhitimisha kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad