HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 22, 2012

Bandari Dar Mabingwa Inter-Ports Games

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akizungumza na wa namichezo wakati wa kuhitimisha michezo ya Bandari inter-ports games ambayo ilifanyika hivi karibuni jijini Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Madeni Kipande akiwa na maafisa wengine wa juu wa TPA.
 Mkuuwa Wilayaya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kikombe cha ushindi wa kwanza kwa mwakilishi wa washindi wa kwanza wa mpira wa kikapu, Kisanta kutoka Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania mara baada kukamilika kwa michezo ya inter-ports iliyofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kikombe cha ushindi kwanza wa michezo ya inter-ports, kapteni wa timu ya mpira wa pete, Judith Ilunda kutoka Bandari ya Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kikombe cha ushindi kwanza wa michezoya inter-ports, kapteni wa timu ya mpira wa miguu, VitalisSalila wa Bandari ya Dar es Salaam.


Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kikombe cha ushangiliaji kwa mwakilishi wa Bandari ya Dar es Salaam ambao waliibuka na ushindi huo mbele ya bandari nyingine wakati wa michezo ya Bandari inter-ports games ambayo ilifanyika hivi karibuni jijini Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba.
Wachezaji wa timu ya Bandari ya Dar es Salaam  wakiwa na vikombe vya ushindi wao mara baada ya kuibuka washindi wa jumla wa michezo ya Bandari inter-ports games iliyofanyika jijini Mwanza hivi karibuni. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad