Naibu
Katibu Mkuu Mtendaji Ofisi ya Rais Kamisheni ya Tume ya Mipango,
Bw. Clinfford K. Tandari, akifuatilia majadiliano yaliyohusu
Utekelezaji wa Mpango wa Istanmbuli kwa nchi maskini maarufu kama
LDGs. Mkutano huo ulifanyika nchini ya Kamati ya Pili ya Baraza Kuu la
67 la Umoja wa Mataifa.
Alipopata
nafasi ya kuchangia utekelezaji wa Mpango huo ( Istambul Plan of
Action) Bw. Tandari pamoja na mambo mengine, alisema Tanzania imekwisha
kuuingiza mpango huo katika Mpango wa Kitaifa wa Maendeleo wa Kila
Miaka Mitano , lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba Tanzania inaondoka
katika kundi la nchi maskini na kuingia katika kundi la nchi zenye
uchumi wa kati ( Middle Income Countries), ikifikapo mwaka 2015.
Akabainisha
kwamba ili kufikia hatua hiyo, Serikali imejiwekee vipaumbele kadhaa
ambavyo vimeainishwa katika Mpango huo wa Miaka mitano.
Akavitaja baadhi ya vipaumbele hivyo kuwa ni Kilimo na Usalama wa
Chakula, uboreshaji wa huduma za Elimu, Afya na huduma za maji na
usafi wa mazingira, maendeleo ya miundombinu ikiwamo ya barabara,
reli, bandari na huduma za nishati.
Akavitaja
vipaumbele vingine kuwa ni usawa wa kijinsia na uwezeshashi pamoja na
kujenga mazingira bora ya biashara na ushindaji wa kibiashara.
Katika hatua nyingine Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Rais
Kimisheni ya Mipango alieleza kwamba Tanzania ingeweza kufikia lengo
lake la kutoka katika kundi la nchi maskini na kuwa kundi la nchi ambazo
uchumi wake ni wakati kabla hata ya mwaka 2015 ikiwa tu washirika wa
maendeleo ya kichumi watatekeleza ahadi zao za kuisaidia Tanzania
zikiwamo zile walizotoa miaka mingi ya nyuma na ambazo hazijatekelezwa
hadi sasa.
Hata
hivyo akasema Tanzania imejidhatiti katika kuhakikisha kwamba
inaboresha makufanso ya mapato yake ya ndani ikiwa ni pamoja na kupanua
wigo wa kodi na kuibua vyazo vipya vya mapato ili kuziba pengo
litokanalo wa wadau wa maendeleo kushindwa kutekeleza ahadi zao.
No comments:
Post a Comment