Kikosi cha timu ya Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mechi ya
Kirafiki kati ya timu ya Umoja wa Mataifa (Blue) na timu ya Wizara ya
Mambo ya Nje (Nyeupe) katika UN Family Day ya maadhimisho ya wiki ya
Umoja wa mataifa kusheherekea miaka 67 ya Umoja huo zikimenyana kwenye
viwanja vya Leaders Club jijini Dar.
Austin
Makani wa UNHCR (mwenye koti la suti) akiwapa mzuka timu ya Umoja wa
Mataifa wakati wa mechi ya kirafiki kusheherekea maadhimisho ya wiki ya
Umoja wa Mataifa ya miaka 67 tangu kuzaliwa kwa shirika hilo.
Hoyce
Temu akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa
mechi kati ya Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa katika
kusheherekea miaka 67 tangu kuzaliwa kwake.
Kiungo
wa timu ya Umoja wa Mataifa akijaribu kumtoka kiungo wa timu ya Wizara
ya mambo ya nje wakati wa mechi ya kirafiki ambapo timu zote mbili
zilitoka sare ya Bao 1-1.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou
(katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya Wakuu wa vitengo vya Umoja
wa Mataifa wakati wa UN Family day kusheherekea miaka 67 tangu kuzaliwa
kwa shirika hilo.
Wakuu
wa Vitengo mbalimbali vya Umoja wa Mataifa wakiongozwa na Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou (mwenye
kofia) wakishindana kuvuta kamba na Wakuu wa vitengo mbalimbali vya
Wizara ya mambo ya Nje ambapo UN iliibuka kidedea katika mchezo huo.
Wizara ya Mambo ya Nje walionekana kuwa wengi na wenye fya na kushindwa katika mchezo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou akipozi na Timu ya Wizara ya Mambo ya nje.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akishangaa jambo na wafanyakazi wenzake.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou na Mwakalishi wa UNESCO Tanzania Bi. Vibeke Jensen.
No comments:
Post a Comment