HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 30, 2012

TRENI YA TAZARA ITAKAYOTUMIKA KWA USAFIRI WA DAR ES SALAAM – PUGU MWAKANGA-KURASINI YAFANYIWA MAJARIBIO.

Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) Mhandisi Abdalla Shekimweri, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo (aliyevaa shati la rangi ya zambarau)katika kituo cha Mwakanga wakati wa majaribio ya mabehewa matatu ya TAZARA yatakayotumika kwa Usafiri wa Dar es Salaam jana. Mabehewa hayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 80 waliokaa kwenye Siti na yanatarajiwa kuanza kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam-Mwakanga na Dar es Salaam-Kurasini kuanzia mwezi Oktoba Mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Mhandisi Omar Chambo akishuka kwenye Kichwa cha treni kitakachofanya Safari zake Dar-Mwakanga-Kurasini mapema mwezi wa kumi.Majaribio ya sehemu ya mabehewa hayo yalifanyika jana. Treni hiyo kwa

Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA)na wa Wizara ya Uchukuzi wakiwa ndani ya Mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio kwa ajili ya Usafiri wa treni Jijini Dar es Salaam jana.
Treni iliyofanyiwa majaribio baada ya kufanyiwa matengenezo ikiwa kwenye muonekano nzuri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad