HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 2, 2012

MKUU WA WILAYA YA KILWA AHAHA KUNUSURU AIBU YA SENSA.

Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega, akizungumza na wakazi wa kijiji cha Pande wilayani Kilwa alipokwenda kutoa elimu ya umuhimu wa kuhesabiwa baada ya wakazi wa kijiji hicho kugoma kuhesabiwa hali iliyomlazimu Mkuu huyo kuhaha vijijini kuhamasisha wananchi wahesabiwe, sikumoja kabla muda wa Sensa kuongezwa.
 Wakazi wa kijiji hicho wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo wakati akielezea umuhimu wakuhesabiwa.
Diwani wa kata ya Pande Mikoma Abdallah Oga, akiwahamasisha wananchi kumsikiliza Mkuu huyo wa Wilaya.


 Said Powa Kilwa.
 
Baada ya Kaya 256 Wilayani Kilwa Mkoani Lindi  kutia dosari  kwenye mbalimbali zikiwemo za  Tingi,
Kilwa Masoko,  Kivinje na Njinjo wilayani humo kwa kukataa kuhesabiwa  kwa madai ya kutokuwapo kipengele cha dini kwenye dodoso la sense Mkuu wa Wilaya hiyo Abdallah Ulega , anahaha vijijijini kuelimisha wananchi huku kwenye baadhi ya vijiji wanaohamasisha wenzao kupinga sense wakitiwa nguvuni.

Siku moja baada ya kutoa taarifa ya hali ya sense kwenye kikao cha Baraza la Maalum la Madiwani wa

Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mkuu huyo alifanya ziara kwenye kijiji cha Pande kuzungumzana wananchi ili wajitokeze kwenye zoezi hilo ambalo likielekea ukingoni kabla ya kuongezwa muda wa siku 7.


Hata hivyo wakazi wakijiji hicho walitoa masikitiko yao kwa mkuu huyo wa wilaya kuwa pamoja na kuwalazimisha kwenda kuhesabiwa lakini wanajisahau mno kwakutokwenda kutoa elimu kwa wananchi jambo ambalo linasababisha sintofahamu kwa wananchi kutokana na kupata taarifa za upande mmoja tu.


Wananchi hao ambao wapo kwenye makao makuu ya tarafa ya Pande pia walihoji kitendo cha kuwanyima haki ya kukutana na tume inayoratibu na kukusanya maoni ya katiba mpya badala yake tume hiyo imepelekwa kwenye kata ambako hakuna uwezekano wa kufika wananchi wengi kutoa maoni yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad