HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 17, 2012

Wadau Wakiwa Mafinga Mkoani Iringa

Mdau Mambo vipi,
Nakuletea picha hizi za jana nilipokuwa Mjini Mafinga kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, nimejifunza kitu hivyo si vibaya tushirikiane. Mara nyingi kilio cha wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake ni joto linalowakera wengi karibia kipindi kirefu cha mwaka, lakini kwa wanaokerwa na joto hilo si vibaya mnapokuwa mapumziko (likizo) mtembelee Mjini Mafinga kupima baridi mwanana inayopatikana eneo hilo kuanzia mwezi wa sita hadi wa nane. 

Leo baada ya mdau mkuu wa mtandao wa Thehabari.com kuwasili Mafinga pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Habari Kuhusu Walemavu (ICD), tulilazimika kutafuta namna ya kuidhibiti baridi iliyokuwa ikivuma eneo hilo asubuhi kabla ya kuendelea na majukumu mengine yaliyotuleta.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad