HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 2, 2012

Rais Kikwete akutana na Rais wa Somalia pia akutana na Mmiliki wa klabu ya Portsmouth Dkt. Sulaiman Al Fahim leo

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Somalia,Mh. Sheikh Shariff Ahmed aliyekutana naye leo june 2, 2012 jijini Arusha.Pamoja na mambo mengine Rais Kikwete na mgeni wake waliongelea hali ya usalama katika nchi hiyo ya pembe ya Afrika na pia akamhakikishia Rais huyo ushirikiano wa kila aina katika kuhakikisha utulivu unarejea nchini Somalia.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mgeni wake Rais wa Somalia,Mh. Sheikh Shariff Ahmed aliyekutana naye leo june 2, 2012 jijini Arusha.PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dkt. Sulaiman Al Fahim wakati walipokutana leo, Jumamosi, Juni 2, 2012, Ikulu Dar es Salaam. Dkt. Al Fahim ambaye ni mwenyekiti wa zamani na mmilikimwenza wa Klabu ya soka ya Portsmouth ya Uingereza yuko nchini kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika uchumi wa Tanzania. Dkt. Al Fahim pia ndiye aliyeongoza mazungumzo na kununuliwa kwa klabu bingwa ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Manchester City na Kampuni ya Arabuni. (Picha na fredy Maro).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad