Yapata Wiki ya Pili Sasa hakujapita Gari la Kubeba Taka katika Mtaa huu kiasi kwamba wakazi wa eneo hili wameamua kukusanya taka zao kwenue Mtaa huu mdogo,hali inayopelekea kuwa kero kwa baadhi ya wapita njia watembeao kwa miguu na hata wale wenye Magari,kwani kadri siku zinavyozidi kwenda ndio taka zinazidi kuongezeka na harufu mbaya inazidi pia.hapa ni eneo la Mikocheni A karibu kabisa na Shule ya Msingi ya Mikocheni A.Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni tafadhalini tunaomba mtusaidie katika hili maana maeneo haya kuna watoto wadogo pia wanaopita njia hii.
Friday, June 22, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment