
Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya (WAMA),Tabu Likoko akifungua semina ya wanawake kutoka vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa vinavyosimamiwa na Taasisi ya (WAMA) kuhusu huduma za Mfuko wa Bima wa Afya NHIF iliyofanyika kwenye viwanja vya Taasisi ya WAMA mapema leo asubuhi jijini Dar es salaam.Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mifuko ya Afya ya Jamii (CHF),Rehani Athumani,Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na Utafiti,Michael Mhando na Mkurugenzi wa Uendeshaji,Eugen Mikongoti.

Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akizungumza jinsi mfuko huo unavyosaidia jamii kupata matibabu wakati wa semina hiyo iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Taasisi ya WAMA jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi mifuko ya Afya ya Jamii (CHF),Rehani Athumani na katikati ni Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na Utafiti,Michael Mhando.

Afisa wa Masoko na Elimu kwa Umma (NHIF) Grace Michael akifuatilia mada katika semina hiyo, kushoto ni Afisa Uraghibishi na Mawasiliano Taasisi ya (WAMA),Philomena Marijani.

Mkurugenzi mifuko ya Afya ya Jamii (CHF),Rehani Athumani (aliesimama) akitoa mada mbalimbali juu ya huduma za mfuko wa bima ya Afya, huku washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza kwa makini.

Washiriki wa semina hiyo wakiandika mambo muhimu yaliyojadiliwa katika semina hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Taasisi ya (WAMA).

Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya (WAMA),Tabu Likoko kulia na Philomena Marijani Afisa Uraghibishi na Mawasiliano Taasisi ya (WAMA) ambao ndiyo wenyeji wa wanasemina wakiwa katika semina hiyo.Picha na Full Shangwe Blog.


No comments:
Post a Comment