HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 26, 2012

Redd's Miss IFM 2012 ni Fina Revocatus

 Mshindi wa Redd's Miss IFM 2012,Fina Revocatus (katikati) akiwa na Mshindi wa Pili,Jane Augustino (kushoto) na wa Tatu Theresia Issaya muda mfupi baada ya kumalizika kwa shindano lao hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Jijini Dar.
 Washiriki walioingia kwenye tano Bora.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Diamond akifanya vitu vyake wakati wa onyesho hilo la urembo  lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Jijini Dar.

Na Mwandishi Wetu

HATIMAYE kitendawili cha nani atafanikiwa kutwaa taji la Redd's Miss IFM na kile cha Redd's Miss Kurasini, kiliteguliwa usiku wa kuamkia leo wakati maeneo hayo yalipofanikiwa kupata warembo wao.

Katika shindano la Redd's Miss IFM kilichofanyika kwenye hoteli ya Blue Pearl, iliyopo Ubungo Plaza Dar es Salaam, mrembo Fina Revocatus alifanikiwa kutwaa taji lililokuwa linashikiliwa na Lucia James.

Katika kinyang'anyiro hicho kilichopambwa na msanii wa Bongo Fleva, Diamond na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki, Jane Augustino alishika nafasi ya pili, huku Theresia Issaya akishika nafasi ya tatu.

Warembo hao kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), wataingia katika kinyang'anyiro cha kumsaka mwakilishi kutoka vyuo vya elimu ya juu katika kuwania taji la Redd's Miss Tanzania baadaye mwaka huu.

Katika shindano la Redd's Miss Kurasini, Flavian Maeda alitwaa taji lililokuwa linashikiliwa na Mwajabu Juma, huku Neema Dolin akishika nafasi ya pili, Lillian Joseph akiwa wa tatu, Angel Joseph wa nne na watano alikuwa Betty Peter.

Kinyang'anyiro hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Equator Grill uliopo Mtoni kwa Aziz Ally, Dar es Salaam na kupambwa na shoo kali kutoka kwa FM Academia na Malkia wa mipasho, Khadija Kopa. Washindi hao watashiriki Redd's Miss Temeke.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's ndio wadhamini wakuu wa mashindano ya Redd's Miss Tanzania kwa muda wa miaka mitatu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad