HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 26, 2012

Biashara ya Panya katika kijiji cha Mandaba nchini Msumbiji

Ukiuangaliwa kwa haraka haraka waweza sema msafara huu ni wakuelekea shambani kwa ajili ya kwenda kuendeleza kilimo kwanza,lakini ukweli ni kwamba jamaa hawa wanelekea porini kuwinda Panya ili baandae warudi town na kuwafanyia makeke ili kuwauza kwa watu mbali mbali.hawa ni baadhi ya wakazi wa kijiji cha Madamba kilichopo kule nchini Msumbiji.
Hapa jamaa wakichimba mashimo wanayohisi kunaweza kuwa Panya ili wakeze kuwakamata kwa urahisi na kwenda kuwapiga bei.Daahhh... hawa jamaa wangekufahamu kwangu ningewashukuru kweli kweli,maana hawa wadudu wanakula kweli nguo zangu pamoja na waya za redio yangu.
Hapa kazi uwindaji porini imeisha tena kwa mafanikio makubwa,maana kila muwindaji anaonekana akiwa na Panya wake.
Wakati mwingine moto hutumika katika kuwapata kirahisi Panya wa kitoweo na biashara,hapa si Msela akionyesha tabasamu la nguvu kupata mzigo kiubwete kabisa.
Mzigo unaivishwa jikoni tayari kwa biashara na kitowewo baadae.
Madogo wakiwa sokoni na Mishkani ya Panya ambapo wanaseka ukigonga na kitu cha Hindi la kuchoma basi mambo yanakuwa mwake kabisa.
Mzigo ukigombewa sokoni
Msela akigonga kitu cha Panya huku jamaa zake mate yakiwadondoka.halafu inaelekea huyu jamaa ni mchoyo sana maana hata hawakaribishi wenzake.
Mzigo ukipigwa sell kwa wasafiri wa mabasi yapitayo katika kijiji hicho cha Mandaba Nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad