Hivi ndivyo ubao wa matokeo unavyoonyesha baada ya kumalizika kwa mchezo wa leo.
Beki wa Taifa Stars,Shomari Kapombe akichuana vikali na Moses Chavula wa Timu ya Taifa ya Malawi huku Makocha wao wakiangalia uwezo wa vijana wao katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Beki wa Timu ya Malawi,Foster Namwera akiondosha hatari iliyokuwa inaelekezwa langoni mwa Timu yao katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Refarii wa Mchezo huo,Oden Mbaga akimuonya Mshambuliaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) baada ya kumchezea rafu Kiungo wa kati wa Timu ya Malawi,James Sangala.
Haruna Moshi Boban yeye na kipa,lakini ilikuwa ngumu kwake kukatiza katika lango la Timu ya Malawi.
Mrisho Ngassa akijaribu kuwatoka Wachezaji wa Timu ya Malawi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Goooo..... daaaaaa...... anapiga fyongo pale na mpira unagonga besela na kutoka nje na kuwa gooooollllliiiii kikiiiiiii....
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars),Mwinyi Kazimoto akiwachachafya mabeki wa timu ya Malawi.
Kocha wa Timu ya Taifa,Kim Poulsen akimpa mawaidha Nahodha wa Timu yake,Juma Kaseja.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa Stars,Haruna Moshi "Boban" akiwachachafya mabeki wa timu ya Malawi katika mchezo wa kirafiki unaoendelea hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Kipindi cha kwanza cha mchezo huu kimemalizika huku timu zote mbili zikitoka bila kufungana.
Haruna Moshi akionyesha makeke yake langoni mwa timu ya Malawi katika mchezo wa kirafiki unaoendelea hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Kipindi cha kwanza cha mchezo huu kimemalizika huku timu zote mbili zikitoka bila kufungana.
Hatari langoni mwa timu ya Malawi.........
Mchambuliaji wa Timu ya Taifa,Mbwana Samatta akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Malawi,Limbikani Mzava katika mchezo wa kirafiki unaoendelea hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Kipindi cha kwanza cha mchezo huu kimemalizika huku timu zote mbili zikitoka bila kufungana.
Wachezaji wa Timu ya Taifa wakitoka uwanja baada ya kumalizika kwa dakika 45 za mchezo huo.
















No comments:
Post a Comment