HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 31, 2012

MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI RUVUMA

Mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Songea ambaye pia ni mkuu wa kikosdi cha 842 KJ Mlale,Meja Mpuku akipokea mwenge wa uhuru mpakani mwa wilaya ya mbinga na songea katika kijiji cha Liganga.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Songea (v) mkoani Ruvuma,Geofrey Guta (kulia) akimkabidhi mwenge wa uhuru kwa mkurugenzi wa manispaa ya Songea,Zakaria Nachoha mara baada ya mwenge wa uhuru kumaliza mbio zake katika halmashauri hiyo.
Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Idd Mponda akimkabidhi mwenge wa uhuru kwa katibu tawala wa wilaya ya Songea,Joseph Kapinga mara baada ya kumalizika kwa mbio za mwenge wilayani mbinga.
Mtawa wa shirika la St Benedictine Peramiho,Hyasinta Shayo akishika mwenge wa uhuru katika kijiji cha Peramiho A Wilayani Songea vijijini.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu Kapt Honest Mwanosa akiweka jiwe la msingi katika jengo la zahanati katika kijiji cha Namatuhi songea Vjijijini jana.ambacho hadi sasa kimegharimi kiasi cha zaidi ya shilingi 200 milioni.
Mama huyu ambaye hakufahamika jina lake mara moja akiwa na furaha na wakimbiza mwenge katika kiijiji cha Namatuhi katika halmashauri ya wilaya ya Songea(v) jana.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kapt Honest Mwanossa akicheza ngoma ya muhambo ambayo ni maarufu kwa wenyeji wa wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma,mara baada ya mwenge kuwasili katika kijiji cha Kigonsera wilayani humo.Picha na Muhidin Amri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad