HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 30, 2012

Mashindano ya Safari Lager Pool kwa Vyuo Vikuu yamalizika mkoani Iringa,Chuo cha St. Agustine watawazwa kuwa Mabingwa wapya

Bingwa wa Singles(mmoja mmoja) wanawake kutoka chuo cha Usimamizi wa Fedha jijini Dar es Salaam (IFM), Modester David akikabidhiwa ngao ya ushindi na Mgeni rasmi Meya wa Manispaa ya Iringa Aman Mamwindi mkoani Iringa mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa Singles(mmoja mmoja) Wanaume kutoka chuo cha St.John, Obira Anyoti akikabidhiwa kitita cha Shilingi laki tatu na mgeni rasmi Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwindi wakati wa kukabdi zawa kwa washindi wa Safari Higher Learning Pool Competition Iringa mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa Singles(mmoja mmoja) Wanaume kutoka chuo cha St.John, Obira Anyoti akikabidhiwa Ngao ya ushindi na mgeni rasmi Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwindi wakati wa kukabdi zawa kwa washindi wa Safari Higher Learning Pool Competition Iringa mwishoni mwa wiki.
Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwindi akimkabidhi kitita cha Shilingi milioni moja na laki tano nahodha wa timu ya IFM, Charles Venance baada ya kushika nafasi ya pili kwa chuo hicho katika mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition yaliyomalizika Mkoani Iringa mwishono mwa wiki.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool(TAPA) Fred Mushi.
Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwindi akimkabidhi kitita cha shilingi milioni 2.5 nahodha wa timu ya timu ya St.Agustine, Jimmy Nicas baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition yaliyomalizika Mkoani Iringa mwishono mwa wiki.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool(TAPA) Fred Mushi.
Ofisa mauzo wa kanda wa Kampuni ya TBL akizungumza na wanafunzi.
Bingwa wa Singles(mmoja mmoja) Wanaume kutoka chuo cha St.John, Obira Anyoti akionyesha ngao yake ya Ubingwa.
Wachezaji wa Chuo cha St. Agustine wakifurahi na kitita chao cha shilingi Milioni 2.5 mara baada ya kuibuka washindi kwenye mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa mwishoni mwa wiki.
Wachezaji wa Chuo cha St. Agustine wakifurahi na Kombe mara baada ya kuibuka washindi kwenye mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa mwishoni mwa wiki.


Na Mwandishi Maalum,Iringa

CHUO cha St.Augustine cha mkoa wa Mwanza jana kilitawazwa kuwa mabingwa wapya wa mashindano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yanayojulikana kama 'Safari Higher Learning Pool Competition 2012 baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 13-9 dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi chuo cha IFM kutoka mkoa wa Dar es salaam katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo.

Fainali za mashindano hayo ambazo zilishirikisha vyuo vinane ambavyo vilikuwa mabingwa katika mikoa yao ngazi ya mikoa ya mashindano hayo na kudhaminiwa na wadhamini wakuu wa mchezo wa pool nchini,Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager,zilifanyikia kwenye ukumbi wa Iringa All Fear mkoa hapa.

St.Augustine kwa kuwa mabingwa wapya wa mashindano hayo walijinyakulia fedha taslim Sh. Mil.2.5 pamoja na kikombe kikubwa cha ubingwa huo.

IFM ambao licha ya kucheza vizuri katika fainali hizo na kujikuta wakipoteza ubingwa huo walizawadiwa fedha taslim Sh.Mil.1.5 kwa kushika nafasi ya pili, chuo cha RUCO kutoka Iringa chenyewe kiliondoka na Sh.Mil.1.3 kwa kushika nafasi ya tatu na St.John's kutoka mkoa wa Dodoma kilishika nafasi ya nne na kupewa Sh. Mil.1.

Vyuo vya MUCCOBS (Kilimanjaro), IAA (Arusha),Mzumbe (Morogoro) na TIA (Mbeya) vyenyewe vilizawadia Sh.500,000 kila chuo ikiwa ni kifuta jasho cha kushiriki fainali hizo.

Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) mchezaji wa chuo cha St. John's cha Dodoma, Obiara David alitwaa ubingwa huo baada ya kumgaragaza vibaya Jackson Raphael wa chuo cha MUCCOBS (Kilimanjaro) magoli 4-0 katika mchezo wa fainali.

Obiara kwa kutwaa ubingwa huo alijinyakulia fedha taslim Sh.300,000 na ngao wakati ambapo Jackson kwa kushika nafasi ya pili alizawadia fedha taslim Sh.200,00, Said Mohamed (RUCO) alishika nafasi ya tatu na kupewa Sh.150,000 na Patrick Peter (IFM) aliambulia Sh.100,000 kwa kushika nafasi ya nne.

Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake), Modesta David (IFM) alitwaa ubingwa huo na kuzawadiwa Sh. 200,000, Remmy Jackson (St.John's) alishika nafasi ya pili na kupewa Sh.150,000, Suchi Anatasia (KCMC) alishika nafasi ya tatu na kupewa Sh.100,000 na Violeth Silas (IAA) aliambulia Sh.50,000 kwa kushika nafasi ya nne.

Aliyekuwa mgeni rasmi katika fainali hizo ni Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad