HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 18, 2012

Wadau wa michezo wafaidi uhondo wa Heineken Champions Planet

 
Meneja Mkuu wa Heineken, Rodney Hensen akiwa na Michael Mbungu na warembo wa Heineken wakati wa uzinduzi wa nyumba ya Heineken Champions Planet iliyopo Masaki jijini ambapo Wadau mbali mbali wa michezo nchini walifaidi uhondo wa nyumba mpya ya kuangalia mechi za ligi ya Mabingwa Ulaya ijulikanayo kwa jina la Heineken Champions Planet iliyopo maeneo ya Masaki jijini.

Wadau hao walishuhudia timu ya Bayern Munich ikiirarua timu ngumu ya Real Madrid kwa jumla ya mabao 2-1 na kujiwekea mazingira mazuri ya kucheza fainali ya mwaka huu ya mashindano hayo.
Wana habari, Majuto Omary na Millard Ayo wakiwa katika picha ya pamoja na warembo Hamissa Hassan ambaye alishiriki Miss Tanzania mwaka jana na marafiki zake kabla ya kuanza kwa mechi hiyo
Mtaalam maalum wa masuala ya media wa kampuni ya Push Mobile, Juila Jessie akiwa pamoja na mchekeshaji maarufu, Evans Bukuku wakibadilishana mawazo katika nyumba ya burudani na michezi ya Heineken Champions Planet iliyopo Masaki jijini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad