HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 18, 2012

Rais Kikwete akiwa nchini Brazil

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil,April 17, 2012 katika mkutano wa Open Government Partnership.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu na mwenyeji wake Rais wa Brazil Mama Dilma Rousseff na wajumbe wengine katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil,April 17, 2012 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership. Kulia ni Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Bi Hilary Clinton.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu wa Georgie Mh Nika Gilauri katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil,baada ya kuhudhuria mkutano wa Open Government Partnership.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Open Government Partnership ukibadilishana mawazo kabla ya ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil. kutoka kushoto ni Waziri katika ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mh Mathias Chikawe, Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mh Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Mahadhi J. Maalim na Msahuri wa Rais (Masuala ya Siasa) Dkt Laurian Ndumbaro.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakipata maelezo kuhusu ukulima wa nyanya wa kisasa katika taasisi ya utafiti wa kilimo (Brazilian Agriculture Research Enterprise - EMBRAPA) walipoitembelea nje kidogo ya jiji la Brasilia.

KWA PICHA ZAIDI 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad