HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, February 12, 2012

ZAIDI YA WANANCHI 5000 WANAKABILIWA NA NJAA MKOANI ARUSHA

Na Mary Ayo,Arusha

WANANCHI zaidi ya 5000 kutoka kata za Nduruma ,Mlangarini na Moshono katika Wilaya ya Arumeru na Moshono manispaa ya Arusha wanakabiliwa na njaa kali kufuatia kitendo cha Jeshi la Wananchi kuwazuia kufanya shughuli zozote katika ardhi wanayodai kuimiliki toka mwaka 1930.

Katika Matangazo hayo wananchi hao hawaruhusiwi kulima ,kujenga nyumba na wala kuokota kitu chochote ndani ya maeneo hayo ambayo ni ya vijiji vilivyosajiliwa kisheria

Hali kadhalika wananchi hao wamedai kunyimwa kuzika maiti za jamaa zao katika eneo hilo huku wengine wakishindwa kukarabati nyumba zao kutokana na hofu ya kuadhibiwa na askari wanaofanya doria katika eneo hilo ili kuhakikisha kuwa maagizo yao yanafuatwa.

Wakizungumza na waandishi wa habari wananchi hao walisema kuwa wametoa vilio vyao kwa muda mrefu kwa viongozi ambao walihidi kulifuatilia haraka lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika .

“Tumeonewa na kudhulumiwa kwa kiwango cha kutisha,serikali yetu imetutendea vibaya kwa kushindwa hata kusikia kilio chetu katika muda wote tuliyopiga kelele za kuomba msaada ,haiwezekani jambo linalohusu maisha ya watu wengi namana hii likapuuzwa kwa kiwango hiki kwa sasa tunaomba mahala pa kuzika ndugu zetu katika vijiji vya jirani”alisema George Mollel mwenyekiti wa Kitongoji cha Kiserian.

Alisema kuwa baadhi ya wazazi wameshindwa kupeleka watoto wao shule kutoakana na kukosa fedha za kulipam karo ya shule .

Kauli hiyo inaungwa mkono na Mzee wa Nyangusi Laanyuni ambaye alisema kuwa watoto wake wamelazimika kuacha masomo kutokana na njaa na hali kuwa ngumu.

“Mimi naiomba serikali iangalie kilio chetu, hawa watoto wasiposoma tutawapeleka wapi katika Dunia ya leo,wengi tumekosa karo.

Naye mmoja wa watu waliochaguliwa katika kamati ya kufuatilia sula hilo Moses Loningo Kivuyo alisema kuwa hali ni mbaya na kwa sasa kitakachofuatia ni wananchi kuchukua sheria mikononi mwao kwa kukaidi matangazo ya Jeshi na kungia katika mashamba yao na kufanya kazi za kilimo na uifugaji.

“Kwa hali ilivyo kwa sasa tunapa serikali siku thelathini itoe tamkoa kuhusu mgogoro huu ,Jeshi letu la wananachi tunalipenda na kuliheshimu ,tunajua wanaotuvuruga ni baadhi ya viongozi wa serikali na Jeshi ambao wana masilahi na eneo hili kwa kjuwa Barbra ya reli inapita na kuna mabaki ya kiwanda cha nyama cha Tanganyika Packers”alisema.

Alieleza kuwa jamii zao zimeshi katika eneo hilo kwa kipindi cha miaka zaidi ya zaidi ya temanini na kwamba jeshi lilifika katika maeneo hayo na kujenga ghala la kuhifadhi vifaa vyao katika eneo hilo katika miaka ya sabini.

“Ndugu mwandishi cha kushangaza zaidi ni kwamba vijiji vyetu vimesajiliwa na kuandikishwa kisheria sasa leo badala ya serikali kuwataka wanajeshi wakae mbali ana ardhi yao wanakubali nguzo za matangazo ya kutunyima kufanya lolote tutaishije kama wanaitaka hii ardhi si wafuate taratibu na kutupa haki zetu kwa mujibu wa sheria “alihoji Kivuyo.

Aidha Mollel alisema jambo la kusikitisha ni hatua ya halmashauri ya Arusha kufika katika maeneo yao kwa njia ya ulaghai na kufanya tathmini ya mali zao kwa njia ya hila.
Alisema kuwa hakuna kiongozi yeyote wa kijiji wala kitongoji aliyeshirikishwa katika zoezi hilo lililofanyika oktoba 2010.

Mwananchi mwingine Elias Ndakusa alisema kuwa watoto wake wameacha masomo kufuatia kushindwa kulipa karo ya shu le huku akisema lishe imekuwa ngumu kutokana na kuzuiwa kulima katika shamba lake.

“Mimi nimezaliwa hapa mwaka 1953 niliwakuta babu zangu wanajeshi walifika hapa mwaka 1975 kujenmga maghala ya silaha lakini eneo hili sii mali yao kuna wakubwa ambao wanhitaji hili eneo kutokana na umuhimu wake kiuchumi”alisema Ndakusa.

Mikael Meibaku alisema kuwa kwa sasa wamefika mwisho na kitakachofuata baad ya siku thelathini ni kuingia katika mashamba yao na kuanza kulima.

“Ni afadhali hawa wanajeshi watuue tufe kuliko mateso haya tunayopata kutokana na kuzuiwa kutumia ardhi yetu kupata kipato halali tuweze kuishi vizuri kama watanzania wengine”alisema Meibaku
.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alikiri kufahamu mgogoro huo na kudai kwamba anawasiliana na uongozi wa serikali ili kutafuta ufumbuzi.

“Siwezi kueleza mambo mengi nina taarifa za madai ya wananchi hao kwani viongozi wao walifika ofisini kwangu na pia waliandika barua ya kulalamika lakini ufumbuzi wake utafikiwa tu siku sii nyingi madai yao siyo ya kupuuziwa hata kidogo”alisema Mulongo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad