HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, February 12, 2012

VODACOM YAWANUFAISHA ZAIDI WATEJA WA M-PESA

Kampuni ya huduma za simu za mkononi inayoongoza nchini leo imetangaza kwa mpigo kwa wateja wake nchini jumla ya ofa 4 zitakazowafanya kuzidi kufaidika, kuwezeshwa na kufurahia zaidi huduma za Vodacom MPESA.

Wateja wa MPESA sasa wamepunguziwa gharama za kufanya miamala kupitia huduma hiyo ambapo sasa miamala itagharimu hadi Shilingi 50 ikiwa ni punguzo la asilimia 75. Wakati huo huo Vodacom ikiongeza kiwango cha bonasi ambacho mteja anaweza kupata akinunua muda wa maongezi kupitia huduma hiyo ya M-PESA hadi asilimia 25 kutoka asilimia 10 ya sasa.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza amesema”Tunatambua ni kwa kiwango gani huduma ya MPESA imekuwa ya umuhimu kwa maisha ya kila siku ya Watanzania, hivyo ni jambo la muhimu pia kwetu kuwapatia ofa zinazoakisi matumizi yao na kuyafanya kuwa rahisi na nafuu zaidi.” “Hii ndio dira yetu kwa mwaka huu na kuendelea” Alisema Bw. Meza.

Ofa nyengine iliyotangazwa na kampuni ya Vodacom Tanzania ni inayomwezesha mteja wa MPESA sasa kuweza kutuma kiasi cha chini zaidi cha fedha cha shilingi 500 kupitia simu yake ya mkononi. Bw. Meza ameielezea ofa hii kuwa inalenga kuhakikisha kila Mtanzania bila kujali hali yake ya kiuchumi anafaidika na huduma bora,salama, ya uhakika na kuaminika ya MPESA.

Aidha, pamoja na ofa hizo, kampuni ya Vodacom imezindua pia promotion ya M-PESA ambapo jumla ya Shilingi 480 Milioni zitashindaniwa na wateja kadri ambavyo wanavyotumia huduma ya M-PESA.

Katika promosheni hii wateja 100 watakuwa wakijishindia zawadi ya fedha taslimu za kitita cha Shilingi 50,000 kwa kila mshindi kupitia droo zitakazochezeshwa kila siku huku droo kuu ya kila mwezi kwa miezi mitatu ikitoa mshindi wa Shilingi 10 Milioni. Promosheni hiyo itadumu kwa siku tisini kuanzia Februari 13, mwaka huu.

“Dhamira yetu ni ya dhati kuhakikisha wateja wetu wanakuwa na furaha wakati wote na huku tukiwawezesha kadri wanayotumia huduma ya MPESA. Tutaendelea kuboresha mfumo wa MPESA sambamba na huduma zinazopatikana katika MPESA ili izidi kuendana na mahitaji halisi ya maisha ya kila siku ya wateja.” Alisema Bw. Meza.

Kupitia huduma ya MPESA mteja anaweza kufanya malipo kwa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo kununua umeme – LUKU, kulipia DAWASCO na DSTV. Aidha huduma ya MPESA inaweza pia kutumika kulipia tiketi za usafiri wa ndani wa anga kwa mashirika ya ndege ikiwemo Precision Air na Coastal Air, kulipia ada za shule, kuweka na kutoa fedha katika akaunti ya benki ya CRDB na huduma nyengine nyingi.

Hakuna shaka huduma ya Vodacom MPESA ndiyo huduma ya kibenki kupitia simu za mkononi inayoongoza nchini ikiwa na mtandao mpana wa mawakala zaidi ya 18,000 walionena nchi nzima mijini na vijijini na inayokua kwa kasi. Ubora na umashauri wa huduma hii unaifanya kampuni ya Vodacom kuzidi kung’ara na kuongoza soko la huduma za simu za mkononi nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad