HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 15, 2012

RAIS KIKWETE KATIKA MSIBA WA MBUNGE WA CHADEMA MAREHEMU REGIA MTEMA NYUMBANI KWA MAREHEMU TABATA

Rais Jakaya Kikwete akimpa pole Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Freeman Mbowe wakati alipokuwa akijiunga na waombolezaji katika msiba wa Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA),Mh Regia Mtema leo nyumbani kwa marehemu Tabata jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akimpa pole mmoja wa ndugu wa Marehemu wakati alipofika katika msiba wa Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA),Marehemu Regia Mtema leo nyumbani kwake Tabata jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Baadhi ya waombolezaji wa msiba wa Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA),Marehemu Regia Mtema leo nyumbani kwake Tabata jijini Dar es salaam.Katikati ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Freeman Mbowe
Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda pamoja na Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda katika msiba wa Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA),Mh Regia Mtema leo nyumbani kwa marehemu Tabata jijini Dar es salaam.Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad