Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii,Dkt. Ramadhan Dau ( wa pili kushoto) akisaini vitabu vya mkataba wa mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ukandarasi ya China Railway Jiangchang Engineering,Bw. Shi Yuan (pili kulia) na Muwakilishi wa Kampuni ya Ukandarasi ya Major Bridge Engineering,Bw. Zhou Yiqiao kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii,Dkt. Ramadhan Dau (kushoto) akibabadilirishana vitabu vya mkataba wa mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ukandarasi ya China Railway Jiangchang Engineering,Bw. Shi Yuan mara baada ya kusaini leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Wengine Pichani ni Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufulli,Waziri wa kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Sadick,Balozi wa Misri nnchini.
Waziri
wa Ujenzi,Mh. John Magufulli akihutubia leo wakati wa hafla ya utiliaji
wa saini wa mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni ambao unatarajiwa
kuanza siku yeyote kuanzia hivi sasa leo kwenye hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.Mkataba huo umesainiwa baina ya Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Wakandarasi kutoka nchini China ambao ni
CHINA RAILWAY JIANGCHANG ENGINEERING CO. (T) LTD na MAJOR BRIDGE
ENGINEERING CO. LTD.
Waziri
wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akihutubia katika hafla hiyo leo
ambapo ametoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi
kuomba kazi za ujenzi huo wa mradi wa daraja la Kigamboni.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick akihutubia katika hafla hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii,Dkt. Ramadhan Dau
akifafanua jambo wakati wa kutoa hotuba yake juu ya mradi wa ujenzi wa
Daraja la Kigamboni unaotarajiwa kuanza hivi karibuni ambao utagharimu
kiasi cha sh. Bilioni 214.6 na utachukua muda wa miezi 36.
Mtaalamu wa Ujenzi wa Madaraja kutoka nchini Misri,Eng. Shwaibu akitoa maelekezo ya namna ujenzi huo utakavyokuwa.
Mtendaji
Mkuu wa Tanroads,Eng. Patrick Mfugale akitoa ufafanuzi wa namna
waliovyoweza kufanya utafiti wa namna mradi huo utakavyofanyika na mpaka
kufikia kumalizika.
Mh. John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na kina sie.
Picha ya mfano wa Daraja hilo la Kigamboni.
Tunashukuru mradi wa ndoto unaelekea kuwa kweli. Onyo kwa watendaji wakianza kuchakachua kwa kudai 10% tumekwisha, tumeumia na mambo kama kawa tutangali tuu hakuna hatua za kuwajibika ndio maana mambo kama kawa. angalieni jinsi waziri Mwanri anavyo ibua madudu huko Kagera ni aibu tupu. UZALENDO UKO WAPI JAMANI. Tunaumizana bila aibu.
ReplyDeleteHakika ni baraka kubwa kwa Tanzania kwani vitu kama hivi tulikuwa tunaona madaraja ya wenzetu huko majuu kwenye picha tu. Ila kama mchangiaji wa hapo juu alivyosema; Uchakachuaji usimamiwe kikamilifu. Nawe mwajiriwa ukiombwa rushwa chukua noti za moto toka TAKUKURU wakome!
ReplyDeleteBaada ya uwanja wa Taifa hili daraja ni namba 2 kuiweka ramani ya Tanzania pazuri zaidi. Reli mpya pana inahitajika kupunguza gharama za usafirishaji nchini!