Naingia zangu Mawindoni huku Manati yangu Shingoni yakining'inia.
Mtu Mzima nikimlia taimingi Cholwe
Aahhh.... si alidondokea hapa,sasa kaenda wapi tena?? au ndio mambo ya nanihii yafanya kazi huku porini.
Hapa nikiachia simkosi,haki ya nani tena vile.
Daahh... Kweli kisicho rizki hakiliki,yaani nimemkosa mara mbili zote...!!!,ngoja niongeze mawe nijaribu tena bahati yangu.
mh staili nyingine za kuchimba dawa kiboko. Unajifanya unawinda kumbe unachafua pori letu huko Bagamoyo.
ReplyDeleteHahahahhaahaha kakaaaa yaani leo nimecheka sana,yaani umenikumbusha mbali sana tuu,ok ukipata TETELE NAMI USINIKOSE!!!!!Angalia usiwindwe wewe tuu.
ReplyDeleteMSHIKAJI ACHA HAYO MAMBO YA KUFUNDISHA JAMII, KUUA NDEGE KWA MANATI. SIO POA HIO! KILA KIUMBE DUNIANI KINA STAHILI HAKI YA KUISHI BILA KUNYANYASWA . KWA NINI UWAWINDE HAO NDEGE WAMAKOSA NINI KAMA UNAHAMU YA NDEGE, KUKU WAPO WENGI TU TENA BEI POA. DUUU MJAMAA LEO NAONA KIDOGO UMENIBOA.
ReplyDeleteHIO SIO MTAA KWA MTAA TENA LEO NAONA UMECHEMSHA TUTAACHA KUANGALIA BLOG YAKO KAMA HUTOJIREKEBISHA WEWE MPIGANAJI WA MAZINGIRA MBONA UNA AANZA YACHAFUA MWENYEWE?
MDAU COPENHAGEN,DENMARK
Yaani mbavu zinavyoniuma ..nimekumbuka wakati nilipkuwa mdogodogo kaka zangu walikuwa wanapenda sana kuwinda ndege kwa manati..Kama Da Rachel hapa juu alivyosema angalia usiwindwe au haya manati yakakurudi:-) Inapendeza siku moja moja kukukumbuka michezo tuliyocheza tulipokuwa wadogo. ukipata usininyime:-)
ReplyDeleteAcha uchu kaka, kindege ukikipiga manati ndio ukalie ugali au? Kama unataka kuwinda chukua bunduki nenda porini....
ReplyDeletehapa sio ulikuwa watafuta pori la kuchimba dawa? Acha kutuvunga kijana.
ReplyDeleteMdau sioni kama Amekosea Toka uishi DENMARK ishakuwa tabu, yeye kaona sawa NDege kuliwa na kutunguliwa na manati kama huko kwenu Europe wanavyowapiga kwa Bunduki Ndege, ukisema ndege asiliwe ale kuku basi kaa juwa kuna nchi zengine nazo hawapendi huyo kuku aliwe na wala asichinjwe na kisu. ukisema sababu kina roho kaa juwa hata mimea ina roho usile majani pia.
ReplyDelete