HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 18, 2012

MINI ZIFF RED CARPET ndani ya New Maisha Club jijini Dar

 Zanzibar International FilmFestival (ZIFF) imeandaa MINI ZIFF RED CARPET katika ukumbi wa New Maisha Clubsiku ya Jumapili tarehe 22 Januari 2012. Wasanii mbali mbali maarufu wa filamuza Kitanzania (Bongo Movies), wasanii maarufu wa Bongo Fleva na wadau mbalimbali wa sanaa nchini wataalikwa kupita katika Red Carpet.

Wasanii wote maarufu wa BongoMovies na Bongo Fleva watahudhuria katika RED CARPET jumapili hii pale NewMaisha Club na baada ya hapo kutakua na onesho maalum ambapo kwa mara ya kwanzaZIFF imeweza kuwaweka wasanii AT na Offside Trick katika jukwaa moja.

MINI ZIFF RED CARPET inaandaliwakufungua kampeni ya “ Nunua kazi halisi ya msanii wa nyumbani ili kukuza tasniaya sanaa nchini/Buy Original Product of our Artists to support the Developmentof Arts in Tanzania". ZIFF imeona umuhimu wa kuanzisha kampeni hii ilikusaidia kusambaza ujumbe huu na uwafikie watanzania wote ambao wengi waowamekua wakinunua kazi zisizo halisi (Pirated Copies) na hivyo kuwanyima mapatowasanii ambao wamekua wakijitahidi katika kujikwamua kimaisha na kukuza tasnianzima ya sanaa hapa nchini.

Katika Red Carpet ZIFF itatoatuzo maalum (Nishani- Medal) kwa Kampuni borailiyotoa mchango mkubwa kwa sanaa ya filamu Tanzania kwa mwaka 2011, Muigizajibora wa kiume kwa 2011, mwigizaji Bora wa kike kwa 2011, filamu bora kwa mwaka2011 na muugizaji bora anayechipukia. Tuzo hizi zitatolewa katika RED CARPETsiku hiyo baada ya Kamati maalum (Panel) ya watu kumi watakaoteuliwa kufanyazoezi maalum la kuchagua watakopata tuzo hizo kutokana na kufanya kazi zaovizuri. Kamati (Panel) hiyo itaundwa na wadau wa karibu wa Bongo movies nawatatoka katika vitengo au mashirika mbali mbali.
Pia MINI ZIFF itaendelea NgomeKongwe Zanzibar tarehe 27 na 28 Januari, 2012, tutaonesha filamu za Kiswahili(Bongo Movies) sita katika screen kubwa ya Amphitheatre kuanzia saa moja usikuna filamu zitakazo oneshwa ni Mr.President ya Steve Nyerere, Big Daddy yaKanumba, Pamoja ya Pastor Myamba, Dj Ben ya J.B, na filamu mpya toka CL& CYproduction.

Filamu zitaoneshwa bure siku ya Ijumaaya tarehe 27, tarehe 28 Jumamosi itaoneshwa filamu moja na kufuatiwa namaonesho ya mavazi kutoka kwa Lucky Creation na Mgece Makory baada ya hapo tamashahili dogo litafungwa na burudani kutoka kwa AT na Offside Trick kwa kiingiliocha shilingi 3,000/= tu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad