Basi la Super Sonic lenye nambari za usajiri T 594 AQC lililokuwa safarini kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea Mkoani Dodoma,limepata ajali maeneo ya Kiluvya mkoani Pwani jioni ya leo mara baada ya kushindwa kulipita lori la mizigolililokuwa mbele yake kutokana na gari nyingine kutokea kwa mbele wakati dereva wa basi hilo akifanya zoezi hilo,hali iliyomlazimu dereva wa basi hilo kulipigiza kwenye lori alilokuwa anataka kulipita huku akipunguza mwendo.Ajali hii imetokea kutokana na uzembe wa dereva wa basi hili kutaka kulipita lori hilo kwenye sehemu ya muinuko ambapo alikuwa hawezi kuona chochote kinachotokea mbele yake.Baada ya kutokea kwa ajali hii,dereva wa basi hili alishuka na kutimua mbio huku abiria waliokuwemo kwenye basi hilo wakimbimbiza bila ya mafanikio kwa aliingia vichakani kwa kuhofea kupigwa na abiria hao ambao walionekana kuwa na hasira kali.hakuna alidhulika katika ajali hiyo.
Hili ndilo lori lililokuwa likipitwa na basi hilo ambalo lilisababisha ajali hiyo.
Baadhi ya mashuhuda wakiendelea kuhadithiana namna ajali hiyo ilivyokuwa na mpaka dereva kuingia mitini.
Baadhi ya abiria waliokuwemo kwenye basi hilo wakiwa wamekaa pembeni ya basi lao hilo huku wakiwa hawajui la kufanya,maana kama ni safari hapo ndio hakuna tena na dereva keshaingia mitini.
Msongamano mkubwa wa magari uliotokana na kutokea kwa ajali hiyo kama unavyoonekana jioni hii.
alikuwa amelewa nini hii ni issue kubwa sana kuwa madereva wakiendesha magari wengi huwa wamelewa
ReplyDelete