Mwezi mmoja tu umepita tangu waziri wa fedha Mustafa Mkulo azindue Airtel Money akiwa na Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor pamoja na Mkurugenzi wa Airtel Money tz Kelvin Twisa,leo wafikia wakala zaidi 10,000.
Huduma ya Airtel money ambayo awali ilijulikana kama ZAP, sasa ni moja kati ya hudumainayoendelea kuenea huku ikineemesha baadhi ya wajasiriamali wadogo wadogo nchini Tanzania kwa kuongeza wigo wa ajira na kipato katika shughuli zao.Airtel Money ni huduma ya kibenki kupitia simu za mkononi ambapo inatolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel yenye mtandao mpana na ulioenea zaidi katika maeneo ya mji na vijijini
Akongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki Mkurugenzi wa Airtel Money Bw Kelvin Twissa, alisema "Huduma ya kutuma na kupoke pesa kupitia simu ya mkononi ya Airtel inajulikana kama Airtel money, huduma hii ya kutuma na kupokea pesa kupitia simu yako ya kiganjani kwa sasa imekuwa ni moja ya sehemu ya mfumo wa maisha ya kila siku kwa watumiaji nchi nzima, hususan kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
Tangu tulipozindua huduma hii kuwa Airtel Money mwishoni mwa mwaka jana leo hii tayari imetimiza zaidi ya Wakala 10,000 (elfu kumi) waliosambaa nchi nzima katika maduka madogo madogo pamoja na wale wafanyabiashara wa kati ambao kwa hali ya kawaida wamejiajiri na tayari wameshaanza kutengeneza faida kubwa kutokana na ile kamisheni wanayoipata kila wanapotoa huduma hii kwa wateja wetu.
Airtel Money ni huduma ambayo ni rahisi na inakidhi mahitaji ya watu wa rika zote katika mifumo yote ya uhamishaji wa fedha" Mfano mzuri ni kama mtu akitaka kuhamisha fedha kupitia njia zozote za kawaida ni lazima asafiri umbali wa kilometa 50, kuja au kwenda katika makao makuu ya wilaya yake ili akutane na watoa huduma ili atume au kupokea fedha katika njia za kawaida tulizozoea awali, lakini sasa huduma hii ya kibenki kupitia simu ya mkononi ya Airtel Money hasa vijijini inaweza kufikiwa kwa umbali wa kila kilometa moja unakutana na DUKA lenye wakala, ndio maana leo tunaona fahari kuwa na zaidi ya mawakala 10,000 muda mfupi toka tulipoizindua huduma hii ya Airtel Money.
Twissa alisisitiza "huduma hii pia inalenga zaidi watanzania wanaoishi vijijini na mijini hususani sehemu ambazo kampuni ya airtel imepanua wigo kwa kuzindua mawasiliano mapya kwa kuwa hakuna mtandao mwingine unaopatikana.
Airtel Tanzania bado tunaendelea na mkakati wa kuweka miundo mbinu ya mawasiliano bora katika maeneo ya vijijini sambamba na kuhakikisha huduma hii ya Airtel money inawafikia wateja wetu walioko kila pande ya nchi yetu na kuwafaidisha.
Airtel Money ni huduma inayowawezesha watumiaji kupokea fedha na kutuma fedha, vilivile inawawezesha kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti zao za benki, aidha kuwatumia muda wa maongezi jamaa zao pamoja na kulipia bili mbalimbali ikiwemo LUKU, DSTV, Dawasco na hata kulipia ada kwa shule mbalimbali zilizokwisha jiunga na mfumo wa ulipaji ada kupitia Airtel Money.
Huduma ya Airtel Money awali ilijulikana kama ZAP na kuzinduliwa kuwa Airtel Money Disemba 6, 2011 ikiwa ni mikakati ya kampuni ya mawasiliano ya Airtel kuboresha na kuongeza huduma zake kwa wateja
wake.
No comments:
Post a Comment