HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 31, 2011

SALAM ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA

SALAM ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA,

TAREHE 31 DESEMBA, 2011

Ndugu Wananchi;

Leo tunauaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012. Naungana nanyi Watanzania wenzangu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na bahati ya kuiona siku ya leo. Wapo ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi ambao hawakujaaliwa kuwa nasi kwa kuwa wametutangulia mbele ya haki. Tuzidi kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape mapumziko mema na sisi tuendelee kumuomba Mola wetu atujaalie rehema na neema tele katika mwaka ujao.

Mapitio ya Mwaka 2011 na Matarajio kwa Mwaka 2012

Miaka 50 ya Uhuru

Ndugu wananchi;

Mwaka 2011 ulikuwa mwaka wa aina yake na wa kihistoria kwa nchi yetu na wenye mchanganyiko wa mambo. Kulikuwa na matukio ya furaha na majonzi na ulikuwa mwaka tuliopata mafanikio mengi na changamoto mbalimbali. Tumeweza kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa heshima stahiki kama nilivyoelekeza katika hotuba yangu ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011. Tumezitumia vizuri sherehe hizo kufanya tathmini ya maendeleo tuliyoyapata tangu Uhuru mpaka hapa tulipo sasa pamoja na kutambua changamoto zilizo mbele yetu.

1 comment:

  1. Hata kumbe haa nao wanakosa fikira nani kamdanganya mhe,, kuawa iwekezaji ni kushika jembe, jufyeka kulima kupalilia na kuvuna . Mbona hayo yamefanywa ila bado nchi ni maskini. Tatizo ni mfumo mbaya wa UONGOZI NDANI YA ccm NA SERIKALI YAKE? wALAU UPATIKANAJI WA KATIBA UNAWEZA KUYATATUA HAYA NA SIO SIASA ZA MAJUKWAANI.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad