HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 12, 2011

AFISA WA TCRA ASHINDA TUZO UINGEREZA

  
Wakati wa kuazimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania hapa Jijini London Ubalozi wetu katika siku ya Ijumaa Tarehe 9 Desemba 2011 ulipata fursa pekee ya kukutana na kumpongeza afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ndg. Semu Mwakyanjala ambaye pia ni mwanafunzi wa shahada ya Pili( Masters Degree in Communication, culture & Media) katika chuo kikuu cha Coventry alieshinda tuzo ya kuandika insha kuelezea jinsi gani nchi ya Ujerumani itakavyokua mwaka 2051.

Aidha Mh. Balozi Kallaghe alimpongeza sana Afisa Semu kwa juhudi zake kwa kufanikiwa kushinda tuzo hii na kuiletea heshima Tanzania Ughaibuni na kuwahamisisha watanzania wote  kusoma na kufanya kazi kwa bidii zaidi. Wakati akiongea na waandishi wa Habari afisa Semu alianza kwa kutoa shukrani kwa familia yake, wafanyakazi wenzake kutoka TCRA na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kumwezesha kufikia hatua aliyopiga leo.
Kutoka Kushoto Naibu Balozi Chabaka, Semu Mwakyanjala na Tim 
Afisa Semu Mwakyanjala akisema machache baada ya kupokea tuzo hiyo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad