HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 25, 2011

Timu ya Pool Ya Taifa yamalizia ziara yake mkoani Tanga,Yaipa kichapo cha bao 13-2

 Nahodha wa Timu ya Pool ya Taifa, Charles Venance akionyesha umahiri wake katika mchezo uliochezwa usiku huu kwenye ukumbi wa Highway jijini Tanga dhidhi ya Timu ya Mkoa wa Tanga.Katika mchezo huo ambao ndio umekamilisha ziara ya Timu ya Taifa kwenye mikoa mbalimbali nchini,imefanikiwa kuupata ushindi mwingine mnono wa bao 13-2 na kudhihirisha kuwa hakuna timu yoyote itakayowasumbua.
Mchezaji wa Timu ya Pool ya Taifa,Anthony Thomas akipeleka mpira shimoni mara baada ya kuupiga kwa namna yake,wakati wa mchezo dhidi ya Timu ya Mkoa wa Tanga uliomalizika usiku huu kwenye ukumbi wa Highway,Jijini Tanga.Timu ya Pool ya Taifa iliimeibuka Kidedea kwa Kuichapa timu ya Mkoa wa Tanga mabao 13-2.
Mchezaji wa Timu ya Pool ya Mkoa wa Tanga,David Curtis akionyesha kiwango wakati wa mchezo wa Timu ya Mkoa huo dhidi ya Timu ya Taifa ulichezwa kwenye ukumbi wa Highway,jijini Tanga.Timu ya Pool ya Taifa iliimeibuka Kidedea kwa Kuichapa timu ya Mkoa wa Tanga mabao 13-2.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad