Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la maofisa wanafunzi aliowatunuku kamisheni jana katika Chuo cha Kijeshi Monduli, Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahi na baadhi ya maofisa wanafunzi aliowatunuku kamisheni jana katika Chuo cha Kijeshi Monduli, Arusha.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu,Dkt. Jakaya Kikwete
akizungumza na Waziri Mkuu wa Kenya,Mh. Raila Odinga wakati alipokuwa
akimsindikiza mara baada ya mazungumzo yao jana jioni jijini
Dar.Kushoto ni Mke wa Waziri mkuu huyo, Mama Odinga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumamosi, Novemba 26, 2011, ametunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Katika sherehe iliyofanyika kwenye Chuo cha Kijeshi Monduli, Arusha, Rais Kikwete alitoa kamisheni kwa maofisa wanafunzi 506 waliofanikiwa kumaliza mafunzo mafupi ya 27.
Kati ya maofisa hao wanafunzi, 69 ni maofisa wa kike na 437 ni maofisa wa kiume na maofisa wote ni wanataaluma wakawa ni pamoja na walimu 101, maofisa mawasiliano ya umma 54, wataalamu wa utawala 48 na wahasibu 167.
Maofisa wengine walitunukiwa kamisheni katika sherehe za leo ni wataalam wa kilimo 14, wahandisi tisa, wanasheria 52, wanahistoria na utamaduni 12, waandishi wa habari 43, wataalam wa ugavi watatu na waataalam wa sayansi ya mazingira watatu.
Wakati huo huo, Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Kenya, Mheshimiwa Raila Odinga.
Viongozi hao wawili wamekutana kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar Es salaam wakati Rais Kikwete akirejea Dar Es Salaam jioni ya jana.
Viongozi hao wamezungumzia masuala mbali mbali yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Kenya na yale ya kikanda.
IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NOVEMBA 26, 2011
wee mpambe wa raisi unatakiwa kuwa makini katika kazi yako kumtizama raisi nguo anazo vaa ona sasa rais anakagua gwaride koti vifungo vingine havijafugwa mara kimefungawa juu kati kiko wazi raisi anaoenekana hayuko smart namna hiyo
ReplyDelete