Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Viongozi na wahitimu katika ngazi mbalimbali kwenye mahafali ya 23 ya chuo kikuu huria cha Tanzania yaliyofanyika jana Bungo Kibaha Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Mhe. Samwel Malechela akimtunuku Shahada ya Heshima Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi kwenye Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika jana Bungo Kibaha. Kulia ni Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Mhe. Samweli Malechela akimtunuku Shahada ya Udaktari wa Falsafa Balozi wa Tanzania Nchini Urusi Balozi Jaka Mwambi, katika Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika jana Bungo Kibaha.kulia ni Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza jambo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Huria cha Tanzania Mhe. Samwel Malechela kwenye Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika jana Bungo Kibaha.Picha na VPO.
No comments:
Post a Comment