HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 27, 2011

Christina Shusho, Bonny Mwaitege, 20%, Glorious Singers… KUMFUNGULIA PAZIA SHIGONGO ARUSHA LEO

Na Mwandishi wetu

Hatimaye lile tamasha lililokuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa la Street University linafanyika leo (Jumapili) kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo wasanii wa muziki wa injili na kizazi kipya Bongo akiwemo Bonny Mwaitege, Abass Hamis Kinzasa ‘20%’, Glorious Singers, Dot Com Generation na wengine wengi watamfungulia pazia mjasiriamali wa kimataifa na mzungumzaji wa kutia hamasa (motivational speaker), Eric Shigongo atakayekuwa mtoa mada kwenye tamasha hilo.

Shigongo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Global Publishers and General Enterprises, atafundisha namna ya kupata wazo la kibiashara, jinsi ya kukuza mitaji, kupata mikopo benki, kujikwamua kimaisha kupitia ujasiriamali na mada nyingine nyingi sambamba na mtoa mada mwenzake, James Mwang’amba kwenye tamasha hilo litakaloanza saa tano asubuhi na kumalizika saa 12 jioni.

Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo, James Mwang’amba tiketi zinapatikana Arusha kwenye Supamaketi ya Shoprite, Summit Centre, Cordial Tours, Hoteli ya Acquiline, Kasi Store, Hoteli ya Kibo Palace na uwanjani (Sheikh Amri Abeid) kwa shilingi elfu tano tu.

Wadhamini wa tamasha hilo ni Kampuni ya Global Publishers Ltd, Malta Guinness, Airtel, Azania Bank, Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPF), Wauzaji na wasambazaji wa vipodozi asili wa Oriflame, Hoteli ya Corridor Springs ya Arusha, Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Wafanyabiashara na Wakulima (TCCIA) na Hoteli ya Kibo Palace ya jijini Arusha.

Wadhamini wengine ni Tripple A Radio (88.5 FM), Sunrise Radio (94.8 FM), Mambo Jambo Radio (93.0 FM), Radio 5 (105.7FM) na Sauti ya Injili Radio (92.2/96.2 FM) zote za jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad