HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 11, 2011

HALI TETE YAZUKA JIJINI MBEYA MUDA HUU,NI VURUGU MTINDO MMOJA

KUTOKA JIJINI MBEYA MUDA HUU NI KWAMBA VURUGU KUBWA SANA LAZUKA  JIJINI HUMO KATI YA WAFANYA BIASHARA NDOGO NDOGO A.K.A WAMACHINGA WANAOFANYA BIASHARA ZAO NJE YA SOKO LA MWANJELWA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI JIJINI HUMO.

VURUGU HIZO ZIMEZUKA MARA TU BAADA YA WAFANYA BIASHARA HAO KUANZA KUWAPIGA KWA MAWE MGAMBO WA JIJI WALIOKUWA WAMEFIKA SOKONI HAPO ILI KUWAONDOA WAFANYA BIASHARA HAO KUFUATIA KAULI YA MKUU WA MKOA WA MBEYA,MH. ABBAS KANDORO YA KUWAONDOA WAFANYABIASHARA WOTE AMBAO WALIKUWA WAMEPANGA BIDHAA ZAO BILA MPANGILIO NJE YA SOKO HILO AMBAO WALIFIKIA HATA KUFUNGA BARABARA YA KUPITA MAGARI KUTOKANA NA UWEKAJI WA BIASHARA ZAO.

ASKARI WA JESHI LA POLISI WAMEFIKA KATIKA ENEO HILO MUDA HUU NA KUANZA KUTULIZA GHASIA HIZO HUKU NA WAO WAKIENDELEA KUPIGWA MAWE NA WAFANYA BIASHARA HAO,HALI ILIYOWALAZIMU KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTULIZA GHASIA HIZO.

KUTOKANA NA GHASIA HIZO,HALI IMEKUWA TETE KWA WAKAZI WA MAENEO YA JIRANI NA ENEO HILO LA SOKO NA KUSABABISHA WATU WENGINE KUKIMBIA MAKAZI YAO KWANI WAFANYA BIASHARA HAO WAMEKUWA WAKIANGUSHA MVUA YA MAWE KWA ASKARI HAO.

TUNAENDELEA KUFATILIA KWA UKARIBU TUKIO HILO NA TUTAENDELEA KUWAHABARISHA KADRI MAMBO YATAKAVYOKUWA YAKIENDELEA JIJINI HUMO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad