HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 10, 2011

taarifa ya msiba Bangalore , Dar es Salaam na Dodoma

Jumuiya ya wanafunzi wanaosoma na kuishi Bangalore, India ( TASABA ) inasikitika kutangaza kifo cha mwanafunzi mwenzetu dada MaryLauren Ndahani Lista (Pichani), aliyekua mwaka wa pili , chuo cha St. George, Banaswadi Bangalore, India

Marehemu alitwaliwa na Mungu akiwa nyumbani kwao Tanzania kwa likizo, na mwili wa marehemu uliagwa jana Dar es salaam kwenda Dodoma kwa maziko.

Jumuiya yetu itafanya ibada maalum ya kumkumbuka na kumuombea mwenzetu siku ya ijumaa (11-11-2011) saa kumi na mbili jioni ( 6pm) nyumbani kwa kiongozi wa jumuiya yetu jimbo ambalo Marehemu alikua akiishi (Banaswadi), Bi. Susan Kavishe, House # 312 3rd OMBR Layout Banaswadi (near St George College ).

Tunawaomba Wanajumuiya tushirikiane vyeka katika kipindi hiki kigumu cha msiba na kuwafariji walioguswa haswa na msiba wakiwemo dada zake walioko Bangalore kwa masomo pia.

Mungu ailaze Roho ya marehemu dada yetu Mary pema peponi

Bwana alitoa, na Bwana ametwaa...Jina lake lihimidiwe

Kwa taarifa zaidi za msiba na misa, tafadhali wasiliana na viongozi wa TASABA

Vice President ... Mr. Anase Stephen ( +919731339875 )
Katibu....... Ms. Edna Stephen ( +919611145774 )
Mweka Hadhina... Mr. Vincent Nkini ( +919731955664 )
Kiongozi wa TASABA - Banaswadi... Ms. Susan O. Kavishe ( +919916683008 )

Imetolewa na:

UONGOZI wa TASABA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad