HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 24, 2011

Changa moto kubwa inayolikabili Bara la Afrika Hivi sasa katika Maendeleo ni kutumia mbinu na Marifa - balozi seif ali iddy

 MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKIONGOZWA NA VIONGOZI WA TAASISI YA MWALIMU NYERERE WAKATI AKIELEKEA UKUMBI WA MKUTANO WA VIONGOZI NA WATAALAMU WA WANAOSHUGHULIKIA KUONDOSHA MIGOGORO BARANI AFRIKA ULIOFANYIKA HOTEL YA MELIA ILIOPO PWANI MCHANGANI MKOA WA KASKAZINI UNGUJA.
 MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKIFUNGUA MKUTANO WA TATU WA VIONGOZI NA WATAALAMU WANAOSHUHULIKIA KUONDOSHA MIGOGORO BARANI AFRIKA UNAO ENDELEA KATIKA HOTEL YA MELIA ILIOPO PWANI MCHANGANI ZANZIBAR.
  WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA TATU WA VIONGOZI NA WATAALAMU  WANAOSHUGHULIKIA KUONDOSHA MIGOGORO BARANI AFRIKA WAKIMSIKILIZA BALOZI SEIF ALI IDDI WAKATI AKIFUNGUA MKUTANO WAO. 
PICHA YA PAMOJA YA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA TATU WA VIONGOZI NA WA TAALAMU WANAOSHUGHULIKIA KUONDOSHA MIGOGORO BARANI AFRIKA MKUTANO HUU UMETAYARISHWA NA TAASISI YA MWALIMU NYERERE WAKISHIRIKIANA NA KITUO CHA HAKI ZA BINAADAMU CHA KIMATAIFA PAMOJA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA NORWAY.

Na Othman Khamis Ame.

Changa moto kubwa  inayolikabili Bara la Afrika Hivi sasa katika kuelekea kwenye Maendeleo zaidi ni kutumia mbinu na Marifa yaliyopelekea kupunguza migogoro ya Kijamii katika baadhi ya Mataifa ndani ya  Bara hili.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Viongozi na Wataalamu wanaoshughulikia Kuondosha migogoro Barani Afrika unaofanyika huko  katika Hoteli ya Melia iliyopo Pwani Mchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Balozi Seif alisema Jamii ya Kimataifa imeshuhudia utatuzi wa Migogoro kadhaa Barani Afrika  hali ambayo kwa kiasi kikubwa imepunguza  Migogoro na hata Mauaji ya Raia wasio na hatia.

Aliwataka Viongozi na Wataalamu hao kutumia fursa nzuri iliyopo ya Amani iliyorejea Barani humu kwa kuweka Mipango bora  itakayoleta faraja zaidi ya ustawi wa Jamii katika miaka ijayo.

“ Tumeshuhudia utulivu wa Kisiasa ilivyorejea ndani ya Bara hili hasa katika Ukanda wa Maziwa Makuu eneo ambalo Sudan na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo { DRC } zilikuwa katika migogoro mikubwa ya Kisiasa  ”. Alikumbusha Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea  matumaini yake  kwamba Ripoti itakayotolewa na Viongozi  hao baada ya kumalizika Mkutano wao itawezesha kujenga mazingira bora ya kudumisha Amani Barani Afrika.

Balozi Seif amezipongeza Taasisi zilizoandaa  Mkutano huo ile ya Mwalimu Nyerere, Kituo cha Hali za Binaadamu cha  Kimataifa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Norway kwa uamuzi wao wa kufanya Mkutano huo Hapa Zanzibar na hasa ndani ya Jimbo lake ya Kitope.

Alisema uwamuzi wao huo haukuwa wa kubahatisha bali imekuja  kwa kuzingatia sifa ya Zanzibar ya amani iliyopelekea kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa { GNU } kufuatia Mgogoro wa muda mrefu uliovihusisha Vyama vya CCM na CUF.

Balozi Seif aliwaeleza Washiriki wa Mkutano huo kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inafanya kazi zake vyema huku ikikabiliwa na changa moto kubwa ya kutekeleza matarajio ya Wananchi wote wa Zanzibar.

Akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Dr. Salim Ahmed Salim alisema yapo Maendeleo makubwa ya kupunguka kwa Migogoro Barani Afrika jambo ambalo limeleta faraja kwao akiitolea mfano nchi ya Sudan.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Haki za Binaadamu bwana David Harland ameipongeza Zanzibar kwa ukarimu wake unaopelekea kupokea Vikao na Mikutano Mzizito ya Kimataifa ndani na nje ya Bara la Afrika.

Wakati wa Mchana akiwa Mkoani Dodoma Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi alikutana wa Uongozi wa Kampuni ya uwekezaji vitega uchumi inayojishughulisha na Mradi wa umeme unaotumia upepo na jua kutoka Nchini India.

Mkurugenzi mkuu wa Kampuni hiyo ya Indomount bwana sudhakar amesema Taasisi yake imepanga kutumia  Jumla ya Dola za Kimarekani Bilioni Moja kati ya Bilioni saba zilizotengwa na waziri mkuu wa Nchi hiyo kusaidia Serikali na Taasisi Binafsi Barani Afrika.

Naye Balozi Seif ameuomba Uongozi wa Kampuni hiyo kuangali Meneo ambalo wanaweza kusaidia kati ya yale yaliyoainishwa na kupendekezwa na Zanzibar katika mipango yake ya Maendeleo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad