HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 5, 2011

MASHINDANO YA NGUMI KULINDIMA WILAYA YA ILALA

ZAIDI ya mabondia 42 wanatarajia kushiriki katika mashindano ya mchezo wa ngumi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba16 mwaka huu jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kocha wa Klabu ya Ashanti ya Ilala, Rajabu Mhamila, 'Super D' alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha Klabu 12 kutoka katika maeneo mbalimbali.

Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala. 

Super D alisema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuendeleza kuhamasisha mchezo wa ngumi nchini ikiwa ni pamoja na muendelezo wa mchezo huo unanaofanywa na Kinyogoli Foundation.

“Tumeandaa mashindano ya ngumi ambayo yatashirikisha vijana mbalimbali na lengo letu ni kuhamasisha mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuuendeleza ili uweze kutuletea faida hapo baadae” alisema Super D.

Kocha huyo aliendelea kusema kuwa vijana watakaoshiriki watakuwa katika uzito mbalimbali kuanzia Unyoya mpaka uzito wa juu.

Aliendelea kusema kuwa pia wanatarajia kushirikisha mabondia wa kike kutoka katika klabu hizo hizo na aliongeza kwa kusema kuwa wanahitaji wadau mbalimbali wajitokeze kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya vijana hao ikiwemo upatikanaji wa maji ya kunywa kwa ajili ya mchezo huo kwa siku hiyo,wenye nia ya kutaka kusaidia au kushiliki kwa kuchangia chochote wanaweza kuja katika ukumbi wa mazoezi uliopo Amana Ilala au kufika Ashanti Boxingi clabu kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na Kocha Mkongwe, Habibu Kinyogoli kwa simu namba hii 0655928298 au unaweza kuwasiliana na Super D kwa simu namba hii O713,0787-406938 Email.superdboxingcoach@gmail.com wadau mbalimbali mnakalibishwa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad