Waandaaji wa Tamasha la Nyama Choma jijini Dar,toka shoto ni Carol Ndosi,Della Ndosi na rafiki yao Omega Assey wakishoo lavu kwa pamoja wakati Tamasha hilo likiendelea katika viwanja vya Posta,Kijitonyama mchana wa leo.
Wakuu wa Kazi,Kulia ni Jeff Msangi wa www.bongocelebrity.com na Shoto ni Dj Bonny Lov wakiwakilisha ndani ya Tamasha la Nyama Choma katika Viwanja vya Posta,Kijitonyama jijini Dar mchana wa leo.
Mdau Mkubwa wa Libeneke la Mtaa Kwa Mtaa (kulia) nae alijumuika na Familia yake katika Tamasha hilo ambalo leo ndio limeanza rasmi na litakuwa likifanyika kila mwaka katika kipindi kama hiki.Kushoto ni mtoto wake.
Wadadazz,kulia ni Rehema a.k.a mama wa make up na shoto ni Della Ndosi mmoja wa waandaaji wa Tamasha hilo la Nyama Choma.Kati ni rafiki wa Rehema.
Mtaalam wa Kutengeneza kilaji cha Wine papo kwa papo pia alikuwepo na hapa akifanya chejo zake katika kutengeneza kilaji hicho ambacho kiliwavutia wengi.
tori kidogo mara baada ya kukata nyama vilivyo.Ni mwendo wa kukata nyama kwa kwenda mbele.Mdau Irene na Mwanae.Jeff Msangi na Bobby ndani ya Nyama Choma Festival at Kijitonyama.
Oda kwa wingi zikitolewa.
Mdau Paul Kirigini akiwa na rafikiye wakigonga nyama vilivyo mchana wa leo katika tamasha la Nyama Choma ndani ya Viwanja vya Posta,Kijitonyama jijini Dar.
Mastelingi katika sekta ya uchomaji Nyama wako makini na kazi yao ili kuhakikisha kila mtu anapata kitu roho inapenda.
Nyama Choma pia Samaki Choma ilikuwepo.
Yaani ilikuwa ni Full Burdani,kama hukufika basi jua umekosa sana uhondo.
Mambo yakiendelea.
Huduma za kujitolea pia zilikuwepo maana kila mtu alikuwa bize na Nyama Choma na vimiminika briiiiddd vilivyokuwepo pando hiyo.
Muziki wa Kutosha toka Mawingu chini ya Dj Bonny Lov uliweza kutawala katika kila kona ya Viwanja vya Posta,Kijitonyana na kumfanya kila aliefika hapo aburudike vya kutosha.
Next time mfanye mashindano ya kula mboga za majani na matunda.
ReplyDeletesifa kubwa ya dada zetu lzm uwe mnene ili upendwe kazi kweli
ReplyDeleteIlikuwa poa sanaa.. Nilikula nyama mpk nikavimbiwa!
ReplyDeleteBig up kwa waandaaji,great work
ReplyDelete