Mchezaji wa timu ya Pool ya Ruaha Iringa, Allen Masebo akicheza wakati wa fainali za mchezo wa Pool Higher Lerning zilizoanza jana mjini Dodoma.
Mchezaji wa timu ya Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM)-kutoka Dar es Salaam,Dicson Mwikola akicheza wakati wa fainali za Pool Higher Lerningza zilizoanza jana Mjini Dodoma.
Mchezaji wa timu ya Chuo cha cha usimamizi wa Fedha (IFM) kutoka Dar es Salaam,Charles Venance akicheza wakati wa fainali za Pool Higher Lerning zilizoanza mjini Dodoma jana.
Muwekahazina wa Chama cha Pool Taifa (TAPA), Zaholo Ligalu akiwapa Semina ya muda mfupi manahodha kutoka kila chuo shiriki katika fainali za Pool Higher Lerning zilizoanza jana Mjini Dodoma.
Wachezaji wa timu Pool ya TAA-Arusha wakifuatilia kwa makini fainali za mashindano ya mchezo huo kwa Higher Lerning yaliyoanza mjini Dodoma jana.
Na Michael Machellah-Dodoma
FAINALI za Mashindano ya Pool Higher Lerning yameanza kwa vishindo Mjini Dodoma kwa kila Chuo kilichoingia fainali katika mashindano kuonekana wanafanya vizuri katika hatua za awali.
Mashindano hayo yamefunguliwa rasmi na mdhamini mkuu wa mchezo huo, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo ambaye aliwataka wachezaji kutoka vyuo mbalimbali kuwa watulivu na kuufanya mchezo uwe wa kuvutia ili kuwafanya hata watazamaji na wapenzi kuupenda mchezo huo.
Shelukindo alisema Kampuni ya Bia nchini (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager wanalengo la kuukuza na kuundeleza mchezo huu nchini Tanzania hivyo ni furaha ya pekee kuona mwaka huu vyuo vingi vimejitokeza kushiriki katika mashindano hayo.
Alisema Oscar,mwaka jana vilishiriki vyuo vya Dar es Salaam tu lakini mwaka huu vyuo kutoka mikoa minane vimeshiriki na leo katika fainali vyuo kutoka mikoa minane vipo katika fainali hiyo.
Hayo ni mafanikio inaonekana tumepiga hatua na kuahidi mwaka kesho TBL kupitia Bia ya Safari Lager wataongeza sapoti zaidi.
Mwenyekiti wa waamuzi wa Taifa, Hashimu Shaweji alisema mpambano ni mkali katika hatua za awali kila chuo kinaonekana kimejiandaa na kuwataka viongozi wa Chama cha Pool Taifa pamoja na Kocha wa timu ya Taifa kutumia muda huo kuangalia kwa makini huweza wakapata wachezaji wa taifa wa kuweza kuisaidia hiyo.
Shaweji akisema tukipata wachezaji wa timu ya Taifa wasomi ni jambo la zuri kwani tutakuwa tunaadaa waalimu wa kuendeleza mchezo huu wa baadae ambao ni wazawa alimaliza shaweji.
Fainali za mashindano hayo zinawakilishwa na vyuo vinane vikiwemo IFM-Dar es Salaam, Ruaha – Iringa, Mist-Mbeya,SUA-Morogoro,St,Agustine-Mwanza,TAA-Arusha,Tumaini –Moshi na wenyejis St.John Dodoma
No comments:
Post a Comment