HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 13, 2011

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NEW YORK NA VITONGOJI VYAKE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal na mkewe, Mama Zakhia Bilal, Balozi Obeni Sefue na Waziri Juma Duni Haji, wakisimama na kuimba wimbo wa maalum baada ya kuwasili kwenye eneo la hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake, Haji Hamis, akizungumza na kutoa utambulisho wa viongozi na wanachama wa Jumuiya hiyo, ambao hadi sasa wamefiki 110.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia Watanzania waishio New York na Vitongoji vyake, wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo nao na kuwatambua, ikiwa ni mara ya kwanza tagu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo.
Baadhi ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Balimi Fc ya Kagera, Henri Rwekagingira (wa pili kushoto) akipozi na dada zake kwa picha wakati wa hafla hiyo.
Mpiganaji Muhidin Sufiani (kati) pia alikuwa ni miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo, hapa akipozi na mchezaji wa zamani wa timu ya Balimi Fc ya Kagera, Henri (wa pili kushoto) na dada zake.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akipiga picha za kumbukumbu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa jumuiya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa jumuiya hiyo baada ya kuwahutubia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa jumuiya.Picha Zote na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad