HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 13, 2011

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI ALIPOTEMBELEA MITAMBO YA KUFUA UMEME YA SYMBION POWER HUKO UBUNGO

Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mama Hillary Clinton akiongea baada ya kutembelea mtambo wa kufua umeme wa kampuni ya Kimarekani ya Symbion Power Ubungo, jijini Dar es salaam jana.
Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja akifafanua jambo baada ya ziara ya Mama Hillary Clinton katika mitambo ya kufua umeme ya Symbion Power iliyopo Ubungo, Dar es salaam
Mjomba Ankal (shoto) akisabahiana na Waziri wa Nishati na Madini, Mh. William Ngeleja wakati wa ziara ya   Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mama Hillary Clinton katika mitambo ya kufua umeme ya Symbion Power iliyopo Ubungo, jijini Dar es salaam.
Mama Clinton akiwa katika mtambo wa kufua umeme wa Symbion Power huko Ubungo jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Bw. Paul Hinks na kushoto wapo Mkuu wa mfuko wa MCC Bw. Daniel Yohannes na Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, Mh Bernard Membe.
Mama Clinton akiwa katika mtambo wa kufua umeme wa Symbion Power.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad