Habari!
Ndugu,
Kwa heshima na taadhima, napenda kukujulisha kuwa baadhi ya wanahabari Watanzania waishio Los Angeles, CA na tuliopo nyumbani (Tanzania ) tumeanzisha gazeti mtandaoni liitwalo 'TheHabari.com', huu ni mtandao wenye madhumuni ya kuwapatia Watanzania habari za Watanzania popote pale walipo duniani, kama ulivyo mtandao wako (blog).
Kwa kuzingatia hilo basi, uongozi wa TheHabari.com ungependa kupata ushirikiano wa ofisi yako, ili kuendeleza gurudumu la maendelea hasa sekta ya habari. Kwenye mtandao wangu nimeweka link yako pia ili kutangazana, bofya www.thehabari.com utaona.
Kama utaridhia ushirikiano kwa leo waweza kunirushia kwako tangazo hili hapa chini:-
LEO KATIKA ‘GAZETI’ LA MTANDAO
*Je, wayajua machungu ya albino Tanzania? Zijue mbinu wanazozitumia kukabiliana na changamoto anuai.
*Shibuda asema; CCM inauchakavu wa fikra. Wataka kujua zaidi ni ki-vipi?
*Wakulima wachoma moto nyumba 23 za wafugaji Sumbawanga.
*Je, wajua milioni 2.6 ya wapiga kura Zimbabwe ni feki?
*Wabunge wa CCM waibana Serikali kuhusu mgawo wa Umeme.
*Marekani yaionya Tanzania juu ya madhara ya Serengeti. Je, wataka kujua undani wa habari hizi, tembelea ‘gazeti’ la mtandao:- www.thehabari.com
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Kwa ufafanuzi kama wahitaji;
email;- mushi@thehabari.com
simu: 0717030066, 0756469470,
Joachim Mushi,
Mhariri Mkuu wa Mtandao Tanzania


No comments:
Post a Comment