HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 24, 2011

VIJANA WAWILI WASAKWA KWA KOSA LA KUMUUA MAMA YAO WA KAMBO MKOANI MBEYA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Advocate Nyombi


Na mwandishi wetu

JESHI la Polisi mkoa wa Mbeya linawatafuta watu wawili Thobias Enock (25) na Jordan Enock (30) kwa tuhuma za kumuua mama yao wa kambo,Bi. Havina John (52) katika kijiji cha Iwindi, Mbalizi Mbeya.

Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya, Bw.Anacret Malindisa aliambia Majira kwa njia simu jana kuwa taarifa za awali zinasema kuwa watoto hao hawakutaka baba yao aishi na mama yao mdogo hivyo kuamua kumpiga kulikosababisha kifo chake.

"Watoto hao walikuwa hawataki baba yao aishi na mama yao mdogo Havina, na baada ya tukio hilo walitoroka na polisi innawatafuta" alisema Mkuu huyo wa upelelezi.

Kaka ya marehemu,Bw. James Ndele alisema siku ya tukio dada yake na mumewe Enock Nswila walikuwa pamoja lakini mumewe alitangulia kurudi nyumbani na kumwacha mkewe.

Alisema baada ya kusubiri kwa muda mrefu mumewe alimfuata alipokuwa amemwacha na kabla ya kufika alikuta kikapu alichokuwa nacho kimetupwa kando kando ya barabara pembeni kukiwa na michirizi ya damu ikielekea porini.

Bw. James alisema alipiga kelele na kuita watu waliomsaidia kufutilia na kumkuta mkewe ameumizwa vibaya na damu zikivuja mwili mzima akiwa hali ikiwa mbaya.

Walipiga simu kuomba msaada wa polisi ambao walifika eneo la tukio na kumkimbiza hospitalini ambako alifariki siku ya pili.

Alisema marehemu Havina ambaye alikuwa akiishi kijiji cha Iwindi alizikwa jana katika kijiji cha Ndangano, Uyole Mbeya

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad